Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amelitaka jeshi la polisi kuhakikisha waliohusika na vitendo vya kumwagia wananchi tindikali wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amelitaka jeshi la polisi kuhakikisha waliohusika na vitendo vya kumwagia wananchi tindikali wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Dk. Shein ametoa kauli hiyo hapa Zanzibar baada ya kumtembelea Padri Joseph Anselmo Mwangamba wa kanisa katoliki parokia ya Mpendae katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja ambapo amekuwa amelazwa tokea jana ambaye alimwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana wakati akitoka katika kituo cha huduma za mitandao-intaneti.

Dk.Shein amesema amesikitishwa na kitendo hicho na kumpa pole Padri Mwangamba ambapo amesema kitendo hicho ni cha ukatili na kisichovumilika na kuongeza kuwa wahusika lazima wasakwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Baada ya kumtembelea Dk. Shein alipata fursa ya kuongea na wanafamilia na waumini wa kanisa waliokuwa hapo hospitali ambapo amewataka kuwa na subira na serikali iko pamoja nao katika kukabiliana na hali hiyo huku padri Mwangamba ambaye kikazi ni mkuu wa kituo cha elimu na vijana kilichopo Cheju amesema hali yake ni nzuri ingawa ana maumivu na uvimbe na anatarajiwa kuwa atapata nafuu..

Mbali ya Dk Shein pia makamu wa pili wa rais Balozi Seif Ali Idd naye alimtembelea wakati wa asubuhi ambapo baadaye padri huyo alisafirishwa hadi Dar Es Salaam kwa matibabu zaidi na uchunguzi wa afya yake ambapo kwa mujibu wa katibu mkuu wa hospitali hiyo Dk. Mohamed Jidawi amesema asilimia 30 ya mwili wake umeathirika

No comments: