LULU AFANYA FILAMU NA MAMA YAKE KANUMBA.


Mwigizaji wa sinema za Kibongo,Elizabeth Michael(Lulu) amecheza filamu na mama wa aliyekuwa msanii wa Bongo Movies,marehemu Steven Kanumba,Frolah Mtegoa iitwayo Mapenzi ya Mungu ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni.

Lulu amepost kava la filamu hiyo kwenye mtandao wa instragram na kuandika kuwa …MAPENZI YA MUNGU....ELIZABETH MICHAEL + FLORA MTEGOHA(MAMA KANUMBA)....STAY TUNED …..

Huku baadhi ya watu wakimpongeza na kumwambia hongera mungu azd kukuangazia .amani yake iwe juu yako.


Hii ni mara ya kwanza Lulu kufanya filamu na Mama Kanumba tangu alipopata matatizo ya kesi ya mauaji ya msanii Kanumba na pengine kuibua maswali kwa mashabiki ni nini kimeongelewa ndani ya filamu hiyo kati ya mtu na ‘mkwewe’.

Filamu hiyo pia imemshirikisha msanii wa Bongo Fleva,Linna Sanga.

No comments: