OPERESHENI YA KUWAKOMBOA MATEKA WANAOSHIKILIWA NA AL-SHABAAB HUKO NAIROBI KUKAMILIKA MUDA MCHACHE KUANZIA SASA..!!
Jeshi la Kenya limefanikiwa kudhibiti
sehemu kubwa ya jengo la kibiashara Westgate na wanaendelea vema na
operesheni ya kuhakikisha wanawakomboa mateka wanaoshikiliwa na
wanamgambo wa kundi la Alshabab ambao walivamia na kuteka eneo hilo
jumamosi mchana.
Msemaji wa jeshi la kenya kanali Cyrus Oguna
amethibitisha operesheni ya kuwakomboa mateka wanaoshikiliwa na
wanamgambo wa Alshabab imefikia hatua ya mwisho na inaweza kutamatika
muda wowote.
Idadi ya watu waliopoteza maisha imeongezeka na
kufikia 69 wakati majeruhi wakifikia 175 kwa mujibu wa serikali nchini
Kenya.Misaada ya aina mbalimbali imeendelea kutolewa ikiwemo zoezi la
uchangiaji damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya majeruhi ambao wengine
wamefanyiwa upasuaji.
Tukio la mashambulizi yaliyofanywa na
wanamgambo wa Al-Shabab kwenye maduka ya westgate nchini kenya limezusha
hofu miongoni mwa mataifa ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki na nchi za Maziwa makuu.
Serikali za Tanzania, Rwanda,
Uganda na Burundi zimelaani shambulio hili na kutoa pole kwa rais wa
Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na wananchi wa taifa hilo ambao wamepoteza
ndugu zao.
Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa kenya kwasasa
inakabiliwa na changamoto kubwa ya kiusalama hali ambayo ni lazima nchi
jirani ziimarishe usalama kwenye mipaka yao.
No comments:
Post a Comment