Bondia
Rashid ‘Snake man’ Matumla amedai endapo itathibitika mdogo wake,
Mkwanda anajihusisha kusafirisha dawa za kulevya atakuwa ameipa fedheha
familia yao.
“Mkwanda
ameipa fedhea familia yetu, hii ni aibu kubwa ukizingatia vitendo hivyo
vinakatazwa si Tanzania tu bali na kwenye nchi nyingine,” alisema
Matumla jana katika mahojiano na gazeti hili.
Mkwanda
ambaye kwa mujibu wa Rashid alipumzika kucheza ngumi miaka kadhaa
iliyopita kutokana na kusumbuliwa na maradhi alikamatwa wiki iliyopita
nchini Ethiopia akiwa na mchezaji wa zamani wa Simba, Joseph Kaniki na
leo watapandishwa kizimbani nchini humo kwa tuhuma hiyo.
“Mimi
mwenyewe nashangaa ni lini amejiingiza kwenye kazi hiyo, hata wakati
anaondoka hakuniaga, mimi kaka yao na familia hatuelewi chochote,”
alisema Matumla.
Alisema
mdogo wake huyo alikuwa amebadilisha uraia na kuchukua uraia wa Sweden
na kuoa hukohuko Sweden licha ya kwamba hapa Tanzania alikuwa amepanga
Mbagala, Dar es Salaam na alikuwa anakuja na kukaa kwa muda na kisha
kuondoka.
“Ni
mwezi sasa umepita sina taarifa naye na hata wakati anaondoka
hakuniaga, nimesikia kupitia vyombo vya habari kitendo cha mdogo wangu
kukamatwa kimenisikitisha mno, siyo siri nimekwazika na ninarudia kusema
hii ni fedheha kwenye familia yetu,” alisema bingwa huyo wa zamani wa
dunia wa WBU. Rekodi zinaonyesha kabla ya kupumzika kwa muda kucheza
ngumi, Mkwanda alishinda mapambano manane (sita kwa KO) alipigwa mara
tatu zote kwa KO alitoka sare mara moja tangu 2004.
SOURCE: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment