Watahiniwa darasa la saba 2013; Watafaulu au watafaulishwa?
Desemba
20 mwaka huu, Serikali ilitangaza matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Darasa
la Saba wa mwaka 2012, yaliyooonyesha kufeli kwa idadi kubwa ya
watahiniwa.
Ni kwa sababu hiyo, Serikali iliamua kuwapa fursa
ya kuendelea na elimu ya sekondari hata watahiniwa waliopata alama chini
ya 100 tofauti na utaratibu ulivyo.
Kwa mujibu wa taratibu za mitihani ya darasa la saba, jumla ya alama
zote ni 250 ambazo hugawanywa katika madaraja matano yaani ni A mpaka E.
Mchanganuo uko hivi: Daraja A huanzia alama 201 hadi 250, B inaanzia
151 hadi 200. Daraja C ni 101 hadi 150 na D inaanzia 51 hadi 100 .
Chini ya alama 50 ni daraja E.
Kwa mtihani wa mwaka jana,
asilimia 40 ya watahiniwa walipata daraja D, lakini bado wakachaguliwa
kujiunga na elimu ya sekondari.
Watahiniwa wapya 2013
Wakati kumbukumbu za matokeo hayo mabaya zikiwa bado katika vichwa vya
Watanzania, kuanzia kesho hadi keshokutwa wanafunzi wa darasa la saba
868,030 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu yao ya msingi
mwaka huu.