VIDEO: TANGAZO LINALOONYESHA PICHA YA MWANAMKE ALIYETEKWA LAZUA KIZAA ZAA...


Ukitizama kwa haraka, ni rahisi kudhani kuwa hili ni tukio halisi na la kweli.
Lakini sivyo. Ni picha iliyokusudiwa kutangaza biashara ya kudurufu uhalisia wa kitu.
Ni picha hii ambayo imeiweka njia panda kampuni moja ya kutengeneza matangazo jimboni Texas, Marekani baada ya 

 kuweka picha (inayoonekana hapo juu) ambayo ilifanana na tukio halisi, ikimwonesha mwanamke aliyelala nyuma ya gari aina ya pick up, huku mikono yake ikiwa imefungwa kwa kamba.



Baadhi ya watu walioona picha hiyo kutokana na kushindwa kung'amua kwa haraka kuwa ilikuwa picha tu na si mtu halisi aliyefungwa, walijikuta wamepiga simu za namba za dharura ili kuwataarifu Polisi kuwa wanadhani kuna mwanamke ametekwa na gari hilo.


Baada ya habari kusambaa kwenye vyombo vya habari, mwenye kampuni hiyo alitoa maelezo kuwa alifanya hivyo si kwa nia mbaya bali kutaka kuonesha uhalisia wa picha za matangazo wanavyoweza kutengeneza.


Ingawaje tukio hilo lilimemwongezea biashara kwa watu kutaka wachapishiwe matangazo yao katika duka lake, bado alipata lawama za kutosha kwa kufanyia tangazo suala ambalo si la utani na halifai.


Ndiyo kusema, 'good business, bad taste', kwamba inawezekana ikawa biashara nzuri ila yenye ladha mbaya na siyo njia inayokubalika kupata fedha kistaarabu.


Mmiliki wa duka hilo aliomba msamaha kwa wote waliokerwa na ubunifu huo.  Video ya taarifa imepachikwa hapo chini.

No comments: