Polisi wakomboa mji uliotekwa na waasi Misri
Wakristo wa Dalga wanasema wamekuwa wakishambuliwa na wapiganaji wa kiisilamu
Maafisa wa polisi wakishirikiana
na wanajeshi wamevamia mji mmoja Kusini mwa Misri ambao ulikuwa
ukidhibitiwa na wafuasi wa aliyekuwa Rais wa taifa hilo Mohammed Morsi
kwa zaidi ya miezi miwili.
Afisa mmoja wa usalama amesema kuwa mamlaka ya taifa hilo imeuteka mji huo wa Dalga uliopo kilomita 300 kusini mwa mji mkuu.
Mji huo ulikuwa chini ya utawala wa
wafuasi hao tangia mapema mwezi Julai baada ya watu hao kuwafurusha
maafisa wa polisi na baadaye kuuteka nyara mji huo.
Wakristo wa dhehebu la Coptic wamekuwa
wakilalamika kwamba wanamgambo wamekuwa wakiwatoza pesa kwa nguvu
,wakisema kuwa hawangeweza kufanya maombi yao vyema kwa sababu ya
usumbufu wa makundi ya walichokiita wahalifu
Maafisa wa Misri, wanawasaka wapiganaji wa kiisilamu kufuatia kuondolewa mamlakani kwa Morsi.
Mamia ya watu waliuawa wakati wanajeshi wa
serikali walipotawanya waandamanaji waliokuwa wamepiga kambi katika
mahema mjini Cairo wakimuunga mkono Morsi.
Mji wa Dalga ummekuwa ukishuhudia maandamano ya
kumuunga mkono Morsi tangu kuondolewa mamlakani kwa Morsi, tangu
wapiganaji wa kiisilamu kuuteka mji huo
No comments:
Post a Comment