Wananchi zaidi ya 200 Mvomero wavamia na kugawana heka 500 za mwekezaji.
Zaidi
ya wananchi 200 wa kijiji cha kibaoni wilayani mvomero mkoani morogoro
hawana maeneo ya kulima baada ya serikali ya kijiji hicho kuuza maeneo
ya mashamba zaidi ya ekari 500 kwa mwekezaji huku wananchi hao
wakitishia kuandamana na kujichukulia sheria mkononi ya kuvamia na
kugawana maeneo ya mashamba hayo
Wakizungumza
wakati wakigawana mashamba hayo wananchi hao wamesema kuwa wamegawana
mashamba kwa wananchi wote ambapo kila mwananchi amepata ekari mbili na
kusema wanashangaa kuona mipaka inawekwa katika maeneo yao kuashiria
kuuzwa kwa eneo hilo bila taarifa huku wakiendelea kukosa maeneo kwa
ajili ya shughuli za kilimo hali inayopelekea kushindwa kulea familia
zao.
No comments:
Post a Comment