JB AWATAHADHARISHA WEMA SEPETU,IRENE UWOYA,AUNT EZEKIEL NA JOHARI WAKAZE BUTI LA SIVYO WATAPOTEA...!!


 

Muigizaji maarufu Swahiliwood Jacob Stephen(JB) amewatahadharisha mastaa wenye majina makubwa katika tasnia ya filamu nchini kuwa wakaze buti baada ya kuanza kupotea kisanii licha ya kuwa na majina makubwa ambapo kwasasa chipukizi kadhaa wanaibuka na kufanya vizuri kuliko wao.
JB aliwataja wazi wazi baadhi ya mastaa wa kike kama vile Wema Sepetu, Irene Uwoya, Aunt Ezekiel na Blandina Chagula(Johari) ambao amesema wameanza kupotea kwenye fani tofauti na mwanzoni huku wengine wakibaki na majina yao tu lakini hawana filamu zozote sokoni kwa muda mrefu.

 
  JB aliyazungumza hayo hivi karibuni katika kipindi cha Take One kinachorushwa NA Clouds Tv. "mimi nimewataja na siogopi, kwani hawa dada zetu wamepotea na kubaki na majina yao tu, nawaomba kama wanataka kutoka kwasasa waendane na mazingira ya sasa" alisema JB
JB alisema kuwa wasanii hao wamekalia kuvaa nguo fupi tu huku wakishindwa kubadilika kutokana na wakati ambapo chipukizi wengi wanaonekana kuwa wabunifu na kuwapita licha ya ukongwe wao.

 

 


Aliongeza kwa kusema kuwa wakati wasanii hao wanaanza kuigiza katika filamu yeye alianza kuigiza kama baba wa lakini kwasasa anafanya vizuri katika sanaa sababu ya juhudi zake kubwa ambazo zimemfikisha alipo sasa.



"mimi kusema kweli kila filamu nilikuwa naigiza kama baba, lakini nikawa najifikiria nitaigiza kama baba mpaka lini, lakini nikajichanganya na nimetoka" alisema star huyo wa filamu za Shikamoo Mzee na Nakwenda Kwa Mwanangu.

No comments: