JAMBAZI BAADA YA KUUAWA NA POLISI LEO ENEO LA SUKITA JIJINI DAR
|
KIKOSI CHA DEFENDER CHA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI KIKOSI CHA POLISI MAGOMENI
|
WAZEE WA KAZI MARA BAADA YA KUMALIZA SHUGHULI YA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI NA KUFANIKIWA KUMUUA MMOJA
|
MOJA KATI YA WATU WANAODAIWA KUPORA FEDHA VINGUNGUTI BAADA YA KUUAWA NA POLISI
|
Jeshi la polisi kikosi cha kupambana na majambazi
kimefanikiwa kumuua mmoja kati ya watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi mara
baada ya kurushiana risasi na polisi eneo la SUKITA jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo limetokea leo saa tano asubuhi maeneo ya SUKITA na taarifa kutoka
eneo la tukio zinasema,watu hao wanadaiwa kupora kiasi kikubwa cha pesa katika
duka moja la jumla na reja reja eneo la vingunguti jijini Dar es Salaam.
Taarifa zinasema majambazi hayo yalikuwa manne na yalikuwa na usafiri wa
pikipiki na mara baada ya kupora wananchi walianza kuyazingira ndipo mmoja wapo
aliyeshika mfuko wa fedha walizopora akaanza kuzirusha kwa wananchi na
walivyoanza kuzigombea pesa hizo ndipo yakapata mwanya wa kutoroka eneo la
tukio.
Hata hivyo taarifa ziliwafikia polisi ambao walikuwa doria na walipewa taarifa
kuwa yanaelekea njia ya sukita na walipowawekea mtego wakanasa,na ndipo katika
harakati za kuwakamata walianza kuwarushia risasi polisi,ndipo moja kati yao,
alipigwa risasi ya kichwa na kufa papo hapo na mengine matatu yakatokomea
kusikojulikana
No comments:
Post a Comment