Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kamishna wa polisi kanda
maalumu ya Dar es Salaam Suleimani Kova amesema ugunduzi huo ulibainika
baada ya uchunguzi uliofanywa na madaktari wa hospitali ya taifa
Muhimbili wakishuhudiwa na polisi pamoja na baadhi na ndugu wa marehemu
ambapo ameelezea marehemu alikutwa na hati za dharura za kusafiria nchi
za nje na kuwa uchunguzi zaidi unafanyika kubaini mtandao mzima wa
usafirishaji wa dawa hizo uliomuhusisha marehemu.
Katika tukio lingine kamanda Kova amesema jeshi
hilo linamshikilia mtu mmoja aliyejifanya kuwa mtumishi wa wizara ya
afya na ustawi wa jamii aliyekamatwa katika hospitali ya taifa Muhimbili
akiwa amevalia mavazi ya kidaktari pamoja na nyara mbalimbali zenye
nembo ya hospitali hiyo kwa lengo la kuwaibia watu.
Kutokana na tukio la ugaidi nchini Kenya kamanda
Kova amesema jeshi hilo limejipanga kuimarisha ulizi maeneo yote yenye
mkusanyiko wa watu wengi na kutoa wito kwa jamii kuendelea kutoa taarifa
kwa jeshi la polisi pindi watakapo baini mtu au kikundi cha watu
wanaowatilia shaka.
No comments:
Post a Comment