MAENDELEO YA KESI YA MASOGANGE HUKO AFRIKA KUSINI NA HII NDIYO RIPOTI YENYEWE.
Mapema Dar es salaam jana Waziri wanchi
ofisi ya waziri Mkuu sera na uratibu wa shughuli za Bunge Wiliam Lukuvi
alisema Serikali inafuatilia kwa karibu kesi zinazowahusisha Watanzania
waliopo nje ya nchi wanaotuhumiwa na biashara ya dawa za kulevya
wakiwemo wanamichezo na wasanii mbalimbali.
Alisema ilikuthibitisha hali hiyo timu
ya watendaji imetumwa nchini Afrika kusini hivi karibu ili kukutana na
kina Masogange kujua undani wa kesi yao na imethibitika kuhusika kweli
na tuhuma hizo ambapo inasadikiwa jana kesi yao imesomwa rasmi na
kusubiri hatua zaidi za kisheria.
Akizungumzia taarifa za kukamatwa kwa
mwanamichezo Kaniki na Matumla Lukuvi alisema taarifa hizo zitatolewa
ufafanuzi zaidi na Serikali baada ya kupokea taarifa za kiofisi kutoka
nchini Ethiopia.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha
kupambana na kudhibiti na dawa za kulevya Godfrey Nzoa alisema kati ya
timu waliokwenda Afrika kusini ni pamoja na yeye mwenyewe ambaye
alifanikiwa kukaa kwa karibu na wafungwa hao akiwemo Masogange na
kubaini kuna siri nzito mgongoni mwa Mwasogange hivyo inahitaji
uchunguzi ili mkono wa sheria uweze kuwagusa wote wanaohusika na kutumia
wasanii katika janga hilo.
“Ni kweli masogange na wenzie
wamekamatwa na dawa aina za Ephedrine ambazo ndio zinazotengeneza dawa
za kulevya na zinaruhusiwa kuingia nchi yeyote kwa kibali malaum kwani
pia zinahusika kutengeneza dawa za kifua na timu iliyotumwa na Serikali
imeweza kuzungumza nao lakini haimaanisha kwenda kwetu gerezani
tunawatetea au tutawasaidia hapana kwakua hawakutumwa kufanya baisahara
hiyo haramu ila tunajaribu kuwa karibu ili kuona wanapata haki zao na
kuweza kubaini waliopo nyuma yao na kweli tumefanikiwa mnyororo ni
mrefu tunaendelea na uchunguzi ili kujua wafadhili na mabosi zao
tunawatiaje mikononi”alisema
Aliongeza kuwa ameshangazwa na kipato
kidogo wanachopata wasanii hao akiwemo Masogange ambapo Afande Nzoa
hakutaka kukiweka hadharani ili kupisha uchunguzi zaidi huku akiongeza
kuwa kufuatia sheri iliyopo wasanii hao kesi zao zitafanyika Afrika
kusini kwakua ndiko walikokamatiwa na endapo kuna mkataba wa
ubadilishana wafungwa Serikali itaangalia njia ya kuwasaidia ili
watumikie vifungo vyao nchini.
No comments:
Post a Comment