Sheikh Ponda Akishuka kwenye basi la Magereza tayari
kuingia Mahakamani Kusikiliza kesi yake inayomkabili katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Mkoani
Morogoro...
Sheikh Ponda
akiwa Chini ya Ulinzi Mkali wakati akiingia Mahakamani kusikiliza kesi
yake inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro.
Sheikh Issa Ponda akiingia Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro leo kusikiliza kesi yake
Wafusi wa Sheikh Ponda wakiwa wakiwa mahakamani leo kusikiliza kesi ya Kiongozi
wao iliyokuwa imetajwa mahama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro.
KATIBU wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu
Nchini, Sheikh Ponda lssa Ponda, amerudishwa mahabusu baada ya kunyimwa
dhamana leo katika kesi yake iliyoendelea kwenye Mahakama ya Hakimu
Mkazi Mfawdhi mkoa wa Morogoro.
Umati mkubwa wa wananchi wengi wao wakiwa waumini wa dini ya
kiislamu ulifurika kwenye mahakama kusikiliza kesi hiyo namba 128 ya
mwaka 2013 ambayo imeahirishwa hadi Oktoba 1 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment