Hollande, Mali kwa sherehe za kumtawaza Rais

 

Ufaransa ilipeleka vikosi nchini Mali kupambana na wapiganaji waliokuwa wameteka eneo la Kaskazini mwa nchi

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande amesafiri hadi mjini Bamako, Mali, kuhudhuria sherehe za kuidhinisha kuchaguliwa kwa rais mpya wa taifa hilo, Ibrahim Boubacar Keita.

Bwana Hollande alituma maelfu ya wanajeshi wa Ufaransa nchini Mali mwezi Januari mwaka huu kupambana na wanamgambo wa kiislamu pamoja na waasi wa kabila la Tuareg ambao waliteka eneo la kaskazini mwa taifa hilo.

Bwana Keita aliapishwa mapema mwezi huu baada ya uchaguzi ambapo aliahidi kuhimiza maridhiano ya kitaifa na utulivu nchini humo.

Mwandishi wa BBC aliyepo mji mkuu wa Mali Bamako, anasema kuwa hali ya usalama katika eneo la kaskazini bado inazua changamoto na mchakato halisi wa amani bado haujaanzishwa.

Takriban wanajeshi alfu tatu wa Ufaransa bado wapo nchini Mali.

No comments: