Chama cha CHADEMA kimesema kuwa madai ya Nape Nnauye kuwa wao walipewa fedha na mfadhili wa nje ya nchi ili kuvuruga mchakato wa katiba mpya unaoendelea nchini ni ya kipuuzi.
Chama
cha CHADEMA kimesema kuwa madai ya Nape Nnauye kuwa wao walipewa fedha
na mfadhili wa nje ya nchi ili kuvuruga mchakato wa katiba mpya
unaoendelea nchini ni ya kipuuzi.
“Madai ya CCM kupitia Nape ni
ya kipuuzi na yanalenga kuwakatisha tamaa wananchi juu ya kazi
inayofanywa na CHADEMA ya kuunganisha nguvu ya umma wa Watanzania dhidi
ya udhaifu wa rais na uzembe wa Bunge linalohujumiwa na CCM katika
mchakato wa Katiba mpya,” alisema John Mnyika
John Mnyika,
ameongeza kuwa madai hayo ya Nape yanadhihirisha kile alichowahi
kukisema bungeni kuwa nchi imefika hapa ilipo kutokana na upuuzi wa CCM.
No comments:
Post a Comment