TUKIO hilo
lililoibua simanzi kubwa kutokana na marehemu kuhitimu Kidato cha Nne
katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Nyihogo, Kahama mwaka jana,
lilijiri saa12:45 Februari 6, mwaka huu.
Kitendo
hicho kilifanyika katika banda la mbuzi lililopo nyumbani kwa kijana
huyo ambaye baada ya kutekeleza mauaji na yeye alifanya jaribio la
kutaka kujitoa roho kwa kisu.
Akisimulia
juu ya tukio hilo, rafiki wa karibu wa Musa ambaye aliomba hifadhi ya
jina lake kwa ajili ya usalama, alisema wiki moja kabla ya tukio hilo,
mtuhumiwa huyo alikuwa akiwatangazia jamaa zake kwamba ana dhamira ya
kumuua binti huyo kufuatia kubaini kuwa anamsaliti kimapenzi.
Muuaji Musa Petro.
“Unajua
Musa anafanya kazi ya kuchuna ngozi za wanyama machinjio ya Wilaya ya
Kahama, alitutangazia dhamira yake hiyo, lakini tulichukulia kauli yake
kama mzaha.
“Alisema anataka kufanya hivyo
kwa sababu amekuwa akitumia gharama kubwa kwa mpenzi wake huyo tangu
walipoanza uhusiano, msichana akiwa kidato cha pili, lakini anatoka
kimapenzi na mwanaume mwingine,” alisema rafiki huyo.
Hata hivyo, inadaiwa baada ya
mtafaruku wa usaliti, wawili hao walipatana na kuendelea na mapenzi,
lakini baada ya mwanafunzi huyo kuhitimu kidato cha nne alibadilika
ambapo mwanaume alisikia kuwa tayari ana mwanaume mwingine kutoka jijini
Mwanza ambaye walikubaliana kufunga pingu za maisha baada ya kumaliza
masomo.
Jessica Elialinga enzi za uhai wake.
Inadaiwa
siku chache kabla ya mauaji hayo, rafiki mmoja wa karibu wa mtuhumiwa
alikutana na marehemu njiani na kumsimamisha kwa lengo la kumweleza
kauli zenye kutishia maisha yake anazozitoa mpenzi wake, lakini binti
huyo hakusimama kumsikiliza.
Baada ya Musa kudaiwa kufaulu
kumchinja mpenzi wake huyo na yeye kujikata koromeo na kuanguka akiwa
ameishiwa nguvu, kijana mchunga mbuzi ambaye wengi katika eneo hilo
humchukulia kama kaka yake Jessica, ndiye aliyekuwa wa kwanza
kumshuhudia Musa akiwa katika hali hiyo.
Alipomhoji
kulikoni, hakupata jibu zaidi ya kushuhudia jitihada za mtuhumiwa huyo
kufungua mlango wa chumbani mwake zikishindikana.
Kijana huyo alitoa taarifa kwa watu ambao walifika na kumchukua Musa na kumkimbiza hospitali ya wilaya kuokoa uhai wake.
Watu waliobaki nyumbani
walifuatilia michirizi ya damu hadi kwenye zizi la mbuzi ambako
walimkuta Jessica ameshafariki dunia baada ya kuchinjwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Everest Mangala alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la
Polisi wilayani Kahama katika Hospitali ya wilaya hiyo anakoendelea
kupatiwa matibabu.
No comments:
Post a Comment