WANAWAKE WAANDAMNA KUDAI SERIKALI IWASAIDIE KUPATA WAUME


Amini usiamini Nigeria ina upungufu wa wanaume wa kuoa!! Kiasi kwamba wanawake wanaotamani kupata wenza na kutengeneza familia wameamua kuchukua hatua. Zaidi ya wanawake elfu 8 walio single jana wameandamana kutokana na upungufu wa wanaume wa kuwaoa.
Lengo la maandamano yao ni kuishinikiza serikali kuwasaidia waolewe, kivipi? (Ndio swali hata mimi nimejiuliza!)
Wanawake waliojikusanya na kuandamana ni mkusanyiko wa 5380 waliopewa talaka, 2200 ni wajane 1200 yatima, na 80 wengine. Wanawake hao wamedai kuwa hawana uwezo hata wa kununua chakula cha siku kwa sababu hawana wanaume wa kuwasaidia ndio maana wanahitaji wanaume wa kuwaoa na kuwasaidia mahitaji yao.

No comments: