Ufaransa yalalamikia mauaji ya raia wake Misri
Polisi wa Misri walikuwa na kibarua kigumu kukabiliana na waandamanaji wakati Morsi alipoondolewa mamlakani
Serikali ya Ufaransa inasema kuwa raia wake mmoja amefariki akiwa amezuiliwa na polisi mjini Cairo.
Duru za usalama nchini humo zimesema kuwa mtu
huyo alichapwa na watu aliokuwa amezuiliwa nao hadi kufariki katika
kituo kimoja cha polisi.
Mtu huyo inaarifiwa alikamatwa baada ya kukiuka agizo la kutotoka nje usiku kucha.
Agizo hilo limewekwa kama sehemu ya sheria ya
hali ya hatari, iliyowekwa na serikali ya kijeshi kutokana na mgogoro
uliozuka baada ya Mohammed Morsi kuondolewa mamlakani na jeshi.
Ubalozi wa Ufaransa unasema kuwa unatafuta
taarifa zaidi kuhusu tukio hilo na hasa kilichosababisha kifo cha raia
huyo wa raia wake ambaye alikuwa ameishi Misri kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment