MWALIMU MKUU ANASWA NA MAGUNIA 6 YA BANGI.
MWALIMU
Mkuu wa Shule ya Msingi Mukubu, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Silidion
Kaiza (43), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na
bangi gunia sita.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi alisema kuwa tukio hilo
lilitokea Septemba 17, mwaka huu, shuleni hapo katika kata na kijiji cha
Muganza majira ya saa tano asubuhi.
Alisema
kuwa raia wema walitoa taarifa kituo cha polisi Rulenge kwamba kuna
mwalimu anajihusisha na biashara ya kuuza dawa za kulevya, jambo
walilohofia kuwa huenda akawaathiri wanafunzi wa shule hiyo kwani
anazihifadhi shuleni.
Kalangi
alifafanua kuwa baada ya polisi kupata taarifa hiyo walifika shuleni
hapo na kumhoji mwalimu Kaiza, na alikiri kufanya biashara hiyo kisha
akawapeleka katika moja ya darasa ambalo alikuwa akitunza bangi hiyo.
Kamanda
alisema kuwa baada ya polisi kukamata bangi hiyo, waliifikisha kituoni
na kwamba mwalimu huyo anaendelea kuhojiwa kisha atafikishwa mahakamani
wakati wowote ili kujibu tuhuma hizo.
Aliwataka
wananchi kuendelea kuwafichua wahalifu wanaojihusisha na vitendo vya
uuzaji wa dawa za kulevya ambavyo vimekuwa tishio kwa taifa.
Source:Boss Ngasa.
No comments:
Post a Comment