MTUHUMIWA AJINYEA MAHAKAMANI WAKATI AKISOMEWA KIFUNGO CHA MIEZI 6 JELA JIJINI DAR..!!
E
Mtu
mmoja amehukumiwa kifungu cha miezi sita jela katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Sokoine Drive kwa kosa la kujisaidia haja kubwa ndani ya Mahakama
wakati akisomewa mashitaka.
Adhabu
hiyo ilitolewa papo hapo baada ya mshitakiwa Hassan Omary (25) kufanya
kitendo hicho aliposomewa mashitaka mengine tofauti.
Hakimu
William Mutaki ndiye aliyetoa hukumu hiyo. Wakati akisomewa mashitaka
sanjari na washitakiwa wengine watatu ya kubughudhi abiria maeneo ya
Kariakoo, Omary inadaiwa alitokwa haja kubwa.
Mwandishi
alishuhudia mshitakiwa huyo akisafisha eneo la mahakamani alikochafua
kabla ya kupelekwa jela. Wengine anaoshitakiwa nao katika kesi hiyo ni
Mohamedi Mussa (20),Hassani Ramadhani (18),Shukuru Adison (26) na Ally
Omary (28).
Mwendesha
mashitaka wa serikali John kijumbe alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi
William Mutaki kuwa washitakiwa walitenda kosa la kuwanyanyasa na
kuwabugudhi abiria ,Septemba 18 ,mwaka huu Kariakoo, jijini Dar es
Salaam. Washitakiwa wengine walirudishwa rumande hadi Oktoba 2,mwaka huu
kesi hiyo itakapotajwa tena.
Katika kesi nyingine, mshitakiwa Jacob Sasita (28) amehukumiwa kifungo cha mwezi mmoja baada ya kukiri kuwanyanyasa abiria .
Sasita
alikuwa miongoni mwa washitakiwa saba waliofikishwa mahakamani kwa kosa
hilo. Washitakiwa wengine ni Ramadhani Juma (38),Abeid Ismail (25),Abuu
Rajabu(25),Salimu Kijimbo (39),Ally Hassani (28),Josephb Chambo (29)na
Fabiani Thomas (28) ambao walikana kutenda kosa baada ya kusomewa
mashitaka.
Mbele
ya Hakimu Mkazi Timoth Lyon, Mwendesha Mashitaka wa Serikari, Richard
Magudi alidai watu hao walitenda kosa la kuwanyanyasa abiria katika
kituo kikuu cha mabasai cha Ubungo ,kabla ya kukamatwa na askari polisi.
Walirudishwa rumande hadi Oktoba 2 mwaka huu kesi itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment