DIWANI ATHUMANI – ACP
---
MNAMO
TAREHE 12.09.2013 MAJIRA YA SAA 19:30HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA
KIBUMBE KATA YA KIWIRA – TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA,
RAPHAEL S/O FRANK, MIAKA 42, KYUSA, MKULIMA NA MKE WAKE SUZANA W/O
FRANK, MIAKA 38, KYUSA, MKULIMA WOTE WAKAZI WA KIBUMBE KIWIRA – TUKUYU
WAKIWA NYUMBANI KWAO WALIGUNDUA KUTOWEKA KATIKA MAZINGIRA YA
KUTATANISHA KWA MTOTO WAO AGNES D/O RAPHAEL, MIAKA 18, KYUSA, MWANAFUNZI
KIDATO CHA NNE SHULE YA SEKONDARI KIWIRA HIVYO JITIHADA ZA KUMTAFUTA
ZILIANZA MARA MOJA USIKU KUCHA BILA MAFANIKIO.
MNAMO
TAREHE 13.09.2013 MAJIRA YA SAA 06:00HRS WAZAZI HAO BAADA YA KUONA
MTOTO WAO HAKULALA NDANI KAMA ILIVYO KAWAIDA WALIAMUA KWENDA KATIKA
KITUO CHA POLISI KIWIRA NA KUTOA TAARIFA YA KUPOTELEWA NA MTOTO. HATA
HIVYO MAJIRA YA SAA 09:00HRS MTOTO WAO AGNES D/O RAPHAEL ALIRUDI
NYUMBANI NA WAZAZI WAKE WALIPOMHOJI JUU YA MAHALI ALIPOKUWA ALIWAJIBU
KUWA ALIKUWA NA MHE DIWANI WA KATA YA KIWIRA [CHADEMA] LAURENT S/O
MWAKALIBULE, MIAKA 28, KYUSA, MKAZI WA KIWIRA – KATI NA KWAMBA WALILALA
KATIKA NYUMBA YA MDOGO WAKE NA DIWANI HUYO AMBAYE JINA LAKE BADO
KUFAHAMIKA NA KUWA KABLA YA KUKUTANA WALIWASILIANA KWA NJIA YA SIMU
YA KIGANJANIMTUHUMIWA AMEKAMATWA, UPELELEZI WA SHAURI HILI UNAENDELEA .
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII HASA WANAFUNZI KUJIEPUSHA NA MADHARA YA KUFANYA
MAPENZI [NGONO] KWANI NI HATARI KWA AFYA ZAO NA PIA KWA MAISHA YAO YA
BAADAE BADALA YAKE WAZINGATIE ZAIDI MASOMO KWA FAIDA YAO , VIZAZI VYAO
NA TAIFA KWA UJUMLA..
No comments:
Post a Comment