Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Erkisongo iliyopo wilayani
Monduli mkoani Arusha, anadaiwa kumchoma kisu katika paji la uso baba
yake mzazi Daudi Msemo baada ya kuonywa kuachana na tabia ya kuchanganya
ngono na masomo.
Hayo yamesemwa na Fatuma Daudi ambaye ni mama
mzazi wa mwanafunzi huyo mara baada kutokea tukio hilo la kusikitisha
hivi karibuni nyumbani kwao Monduli ambapo denti alipofikishwa polisi
alisema alifanya kitendo hicho kwa sababu baba yake alitaka kumbaka.
“Binti
yetu huyu amekuwa akibadilika tabia na mara nyingi tumekuwa tukimuonya
aache vitendo vya umalaya akiwa mwanafunzi lakini bado amekuwa
akiendeleza tabia yake hiyo ambayo sisi wazazi tumeona ni kudharau
maagizo yetu,” alisema Fatuna.
Aliongeza kuwa, tabia hiyo ilikuwa ikimfanya mwanafunzi huyo kuchelewa kurudi nyumbani na wakati mwingine kutorudi kabisa.
Mama
huyo alisema, kutokana na tabia hiyo waliamua kumdhibiti ili aache
lakini matokeo yake alimchoma kisu baba yake na akamsingizia alitaka
kumbaka hali iliyowalazimisha polisi kuwaweka ndani wote.
Fatuma
alikwenda mbali zaidi kwa kuwaomba baadhi ya wanajeshi ambao wana
uhusiano wa kimapenzi na binti huyo waache kwa kuwa ni kinyume cha
maadili na mwanaye bado ni mwanafunzi wa kidato cha nne.
Maelezo
ya denti huyo yalimfanya baba mzazi kuahidi kujiua baada ya kutoka
kituoni hapo akidai amedhalilishwa sana, hali iliyowafanya polisi kuamua
kuendelea kumshikilia licha ya kwamba walishamruhusu kutoka baada ya
mkewe kumtetea.
Afisa mmoja wa jeshi la polisi ambaye hakutaka kuandikwa jina lake kwa kuwa siyo msemaji alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Tunaendelea
na uchunguzi na wote wawili, baba na mwanaye tunawashikilia ili kubaini
chanzo cha kutokea kwa tukio hilo, baada ya uchunguzi maelezo zaidi
utapewa na kamanda wa mkoa afande Liberatus Sabas, kwani ndiye msemaji
wa jeshi mkoani hapa,” alisema afisa huyo
No comments:
Post a Comment