England haitashinda kombe la dunia'


Greg Dyke

Mwenyekiti wa chama cha soka nchini Uingereza Greg Dyke, amesema kuwa hana matumaini ya Uingereza kushinda kombe la dunia nchini Brazil mwaka ujao.

Akiwahutubia waandishi wa habari mjini London, alitaka timu ya Uingereza kujitahidi kufika nusu fainali ya kombe la Uropa mwaka 2020 na kuwa na matumaini ya kushinda kombe la dunia mwaka 2022.

Aliambia BBC kuwa: "haimaanishi kuwa hawawezi kufanya vyema nchini Brazil, muhimu wafuzu tu.''

"sidhani kama hata tunaweza kushinda kombe la dunia nchini Brazil.''

Uingereza wanakabiliwa na kibarua kigumu katika siku chache zijazo wakati watakapojaribu kufuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia nchini Brazil mwaka ujao.

Kikosi cha kocha Roy Hodgson, waliobanduliwa nje ya michuano ya robo fainali ya mataifa ya Ulaya mwaka 2012, watacheza na Moldova katika uwanja wa Wembley siku ya Ijumaa. Waliicharaza timu hiyo mwaka jana mabao matano bila, baadaye Jumanne watasafiri kwenda Ukrain

Kwa sasa wanashikilia nafasi ya pili kwenye kundi H, alama mbili nyuma ya Montenegro, ambao wamecheza mechi moja zaidi ya Uingereza.

Hata hivyo Dyke ana matumaini makubwa kuwa England itafuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia Brazil. Wakati wa mwisho kwa England kushinda kombe la dunia ilikuwa mwaka 1966.

No comments: