AIBU KWA HUYU MSANII WA FILAMU ZA BONGO"Irene Uwoya akamatwa na polisi kwa wizi wa simu aina ya iPhone 5.'
MSANII
aliyewahi kutamba kisha kuporomoka kwa kasi katika tasnia ya filamu
nchini Tanzania kwa sababu ya tabia zake chafu, Irene Uwoya, amefikishwa
Kituo cha Polisi Msimbazi kwa wizi wa simu aina ya iPhone 5.
Kwa mujibu wa habari za kipolisi, mmiliki wa simu hiyo ni mwanamme aliyejulikana kwa jina la Mohammed Marjey, mkazi wa Dar.
Uwoya
ambaye siku hizi anajitutumua kwa kuanzisha kipindi kwenye runinga moja
ya Bongo baada ya kushindwa kwenye filamu, alidakwa na askari wa Kituo
cha Polisi Msimbazi, Dar baada ya kusakwa usiku na mchana kwa kutumia
kumbukumbu ya jalada la kesi namba MS/RB/8522/13 WIZI KUTOKA MAUNGONI.
Simu aina ya iPhone 5 kama inayodaiwa kuibiwa na Uwoya.
Akizungumza
na mwandishi wetu, Mohammed alisema simu hiyo aliinunua mwaka huu
kwenye Duka la Grande Center jijini New York, Marekani alikokwenda kwa
shughuli zake.Akasema Agosti 22, mwaka huu alirejea Bongo akiwa na simu
hiyo ambayo ni toleo jipya la mwaka huu.
“Nilirejea
hapa nchini nikiwa na simu hiyo. Tena unajua simu yenyewe ni ya kisasa,
toleo la mwaka huu,” alisema Mohammed.Alisema Agosti 23, mwaka huu,
akiwa kwenye gari katika Makutano ya Barabara ya Uhuru na Mtaa wa
Nyamwezi, Kariakoo, Dar aliibiwa simu hiyo na mtu asiyemtambua.
“Nilikwenda
Polisi Msimbazi kuandikisha maelezo na kupewa RB hiyo. Lakini nilitumia
njia ya kitaalam kufuatilia, nikagundua simu yangu inatumiwa na mtu
anayeitwa Peter, nikampigia simu kumwambia lakini hakuweka wazi
aliipataje?
Mohammed
alisema baada ya dakika kumi, alipigiwa simu na Uwoya na kumchimba
mkwara kuhusu simu hiyo huku akisema ni yake yeye, jambo ambalo
lilimshangaza jamaa huyo.
“Nilirudi
Msimbazi na kuwaambia ndipo polisi wakaanza kazi ya kumsaka ili
wamkamate.Amekamatwa akiwa na hiyo simu yangu,” alisema.
Inadaiwa
kuwa polisi walimuuliza Uwoya alikoipata simu hiyo ambapo alisema
alipewa na jamaa yake wa Afrika Kusini huku mlalamikaji huyo akitoa
risiti ya kununulia.
Baada
ya kumaliza kuhojiwa kituoni hapo, Uwoya alitolewa kinyemela kwa mlango
wa nyuma ili waandishi waliopiga kambi nje ya kituo hicho wasimfotoe.
No comments:
Post a Comment