WALIOMBAKA MWANAFUNZI NDANI YA BASI WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA.
Wanaume wanne jana wamehukumiwa kifo kwa kuhusika na shambulio la ubakaji na mauaji ya msichana kwenye basi mjini Delhi.
Jaji
Yogesh Khanna, ambaye aliwatia hatiani wanaume hao kwa shambulio la
ubakaji na 'kusababisha' mauaji mapema wiki hii, alikataa ombi la
mwanasheria wao la kuwapunguzia adhabu wateja wake hao.
Shangwe
zililipuka kutoka kwenye umati wa watu nje ya mahakama hiyo ya Delhi
pale wanasheria walipotoka nje kwa kasi na kutangaza hukumu hiyo
iliyotolewa kutokana na shambulio hilo la Desemba mwaka jana, ambalo
liliibua maandamano makubwa kote nchini India na midahalo kadhaa kuhusu
uhalifu dhidi ya wanawake.
"Hii imeshitua jamii nzima ya wapenda amani," Jaji Yogesh Khanna alisema, akiwahukumu wanaume hao adhabu ya kunyongwa hadi kufa.
"Katika
nyakati hizi huku uhalifu dhidi ya wanawake ukiongezeka, mahakama
haziwezi kugeuka vipofu mbele ya makosa hayo ya kutisha."
Hukumu hiyo ilikuwa moja ya vipimo vikubwa kabisa kwa miaka kadhaa ya mtazamo wa kweli kinzani ya India kuelekea hukumu ya kifo.
Majaji
wa nchini humo wanatoa, kwa wastani, hukumu 130 za kifo kila mwaka
lakini India imeshaua watu watatu tu katika miaka 17 iliyopita.
Pichani
ni nyuso za watu wanne walio hukumiwa adhabu ya kifo kwa ubakaji na
mauaji ya kikatili ya mwanamke kijana yaliya fanyika kwenye basi mjini
New Delhi , Desemba mwaka jana.
Licha ya kusita kwake
kutekeleza hukumu hizo, mwaka jana India ilipiga kura dhidi ya
upitishwaji muswada wa Umoja wa Mataifa uliotaka ruhusa ya kusitishwa
kwa muda adhabu za kifo.
Wanasheria wa watuhumiwa wote wanne
walisema watakata rufani, kitu kinachomaanisha utekelezwaji hukumu zao
unaweza kuwa miaka kadhaa ijayo. Kesi hii itakwenda katika Mahakama za
Juu na kisha Mahakama Kuu.
Endapo zitathibitisha hukumu hizo, uamuzi wa mwisho utamtegemea Rais, ambaye ana mamlaka ya kufanya huruma.
Mmoja
kati ya wanne hao, mwalimu wa gym Vinay Sharma, alimwaga machozi wakati
akitolewa nje ya mahakama hiyo, ambako polisi wakiwa na vifaa vya
kukabiliana na ghasia walijipanga kuzuia umati mkubwa wa wananchi.
Mwathirika
huyo, ambaye alibakwa kwa saa moja na kujeruhiwa kwa nondo ndani ya
basi lililokuwa kwenye mwendo, amekuwa alama ya hatari wanazokabiliwa
nazo wanawake katika nchi ambayo ubakaji unaripotiwa kwa wastani wa kila
dakika 21 na mashambulio ya tindikali na kesi za kukera yameshika kasi.
Mwanamke
huyo, ambaye ametokea katika familia ya maisha ya kati na kufanya kazi
kwenye kituo cha mawasiliano wakati akiwa anaendelea na masomo,
hajatajwa kutokana na sababu za kisheria, lakini vyombo vya habari vya
India vimempachika jina la Nirbhaya, neno la Kihindi linalomaanisha
asiye na hofu.
"Leo tunaweza kupumua kidogo kirahisi," alisema
mama wa mwathirika huyo, ambaye alimkumbatia ofisa mmoja wa polisi nje
ya mahakama hiyo baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo. "Natumaini hukumu
hiyo itawatisha watu kufanya makosa kama haya kwa siku za usoni."
Mawakili wa utetezi wameiasa mahakama hiyo kupuuza walichosema kimezagaa na shinikizo la kisiasa kutoa adhabu hiyo kali zaidi.
"Huu sio ushindi wa ukweli. Ila ni pigo kwa haki," wakili wa utetezi A.P. Singh aling'aka kwa jaji wakati hukumu hiyo ikisomwa.
"Jaji amechukua uamuzi huo chini ya shinikizo la kisiasa bila kujali uhalisia," aliwaeleza waandishi baadaye.
Waziri
wa Mambo ya Ndani nchini humo, Sushilkumar Shinde, alikanusha kwamba
kulikuwa na muingilio wa kisiasa, akisema: "Hakuna mamlaka yoyote ya
sheria inayoathiriwa na serikali."
No comments:
Post a Comment