Vincent Kigosi ‘Ray'
KIMENUKA! Waigizaji wenye majina makubwa Bongo, Blandina Chagula
‘Johari’ na Chuchu Hans wanadaiwa kuchapana kisa kikidaiwa kuwa ni penzi
la mwigizaji ‘kaka mkubwa’, Vincent Kigosi ‘Ray’, Amani limenyetishiwa
mkanda kamili.
Blandina Chagula ‘Johari’
TUHUMA
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho ni rafiki wa
karibu wa wasanii hao, tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita
ndani ya Ofisi za RJ Productions, zinazomilikiwa kwa ubia wa Ray na
Johari zilizopo Sinza-Mori jijini Dar ambapo Johari alikuwa akimtuhumu
Chuchu mambo mazito ya kimapenzi kwa Ray.
Shushushu huyo alitonya
kuwa, siku ya tukio Johari na wasanii wenzake walikuwa wakirekodi filamu
ndani ya hoteli moja (jina tunalo) iliyopo jirani na ofisi hizo ndipo
alipofikishiwa umbeya kuwa Chuchu yuko kwenye ofisi hizo ‘akijiachia’ na
bosi mwenzake (Ray), jambo lililotia ganzi moyoni mwa mdada huyo.
Chuchu Hans.
MCHEZO MZIMA
‘Kikulacho’ huyo aliendelea kudai kuwa baada ya
Johari kupata habari hizo, bila kujiuliza wala kuvuta subira, ‘alisaga
soli’ hadi maeneo hayo.
“Alipofika aliingia ndani moja kwa moja na kumvamia Chuchu huku akimshushia kipigo chenye ujazo,” kilidai chanzo hicho.
Alidai kuwa katika timbwili hilo, Chuchu naye alifurukuta ndipo
wakazichapa laivu kabla ya Ray aliyekuwa nje kusikia na kuwahi kuokoa
jahazi.
“Unajua kilichomshtua Ray ni kilio cha Chuchu aliyekuwa akiomba msaada baada ya kuzidiwa na Johari,” kilidai.
Chanzo kilidai kuwa aliingia ndani akiwa amefura na kufoka lakini
alikuwa ameshachelewa kwani tayari Johari alikuwa ameshaugeuza bucha
mwili wa Chuchu.
Ilidaiwa kuwa baadaye Ray alimtoa nje Johari akimtaka kuwa mbali na Chuchu.
SINEMA YA BURE
“Ilikuwa ni bonge la soo, watu walijaa sana, baadaye Ray alimtoa Johari nje huku akimfokea.
“Unaambiwa Johari alikuwa akikimbia na Ray kumfukuza, jambo lililovutia
watazamaji wa sinema hiyo ya bure,” alisema mpashaji wetu.
JOHARI, CHUCHU WASAKWA
Baada ya kuzinyaka taarifa hizo, gazeti hili liliwasaka Johari na Chuchu kwa nyakati tofauti.
JOHARI AKIRI
Kwa upande wake Johari alikiri kutokea kwa kasheshe hiyo.
“Ni kweli lakini nani amekuambia? Unajua kilichoniudhi mimi ni maneno
machafu ya huyu dada (Chuchu) anavyotamba kwa watu kuwa amenipokonya
mume, wakati hakuna ukweli juu ya hilo, nilishikwa na hasira sana ndiyo
maana nikaamua kumpa somo kidogo.
“Inaniuma kwa sababu mimi na Ray
tumetoka mbali sana hadi kuisimamisha RJ. Tulikuwa hatuna kitu kabisa
tukaungaunga huku na kule hivyo Chuchu anapaswa kutambua hilo. Asitake
kunikumbusha vitu vingi kwa sababu tuliteseka sana,” alisema Johari kwa
uchungu.
VIPI BADO ANAKWENDA RJ?
“Tangu ile ishu itokee sijaenda RJ kwa
sababu Ray alinifukuza eti kisa Chuchu. Usiniulize muafaka wa hili jambo
kwa sababu hadi sasa sina majibu ya moja kwa moja kuna vitu naviweka
vizuri,” alisema mwanadada huyo.
HUYU HAPA CHUCHU
Kwa upande wake Chuchu aliruka kimanga kuwa hakuna ishu kama hiyo.
“Aaah, jamani sina cha kusema juu ya hilo, nikiwa tayari nitawaambia.
“Kinachonishangaza kila Johari na Ray wakigombana huwa natajwa mimi.
Yaani sijui hata haya mambo yanatokea wapi,” alisema Chuchu.
RAY
Gazeti hili lilipomtafuta Ray kutaka kujua ukweli wa ishu hiyo, bila kujibu ndiyo au hapana, alimjia juu mwandishi:
“Sikia Brighton (mwandishi), hili jina nimelitafuta kwa miaka mingi. Nakuomba usiandike habari hiyo, sielewi chochote.
“Ugomvi wao siujui na wakigombana waache kunitaja, waeleze sababu zao
za kugombana siyo kunitajataja mimi,” alisema Ray na hata alipoulizwa
uhusiano wake na wanawake hao aliishia kujiumauma bila kutoa majibu ya
kueleweka.
HALI NI MBAYA
Habari za kina zilidai kuwa hali ni mbaya kati ya
mastaa hao ambapo mashabiki wao waliozungumza na gazeti waliiomba Kamati
ya Nidhamu ya Bongo Movie kuingilia kati ugomvi huo ili kutafuta
ufumbuzi.
Source:GPL
No comments:
Post a Comment