Roy Hodgson atetea England
England ilienda sare tasa na Ukrain matokeo ambayo yamewakera wengi
Meneja wa timu ya Uingereza Roy
Hodgson, amesema aliridhika na walivyocheza wachezaji wake walipojitosa
katika michuano ya kuwania kombe la dunia.
England ilienda ilimaliza mchezo kwa sare tasa dhidi ya Ukraine kwenye mechi iliyochezwa mjini Kiev
Kikosi cha Hodgson kinasalia juu
katika kikundi cha H na kitafuzu ikiwa kitashinda mechi zao mbili za
kufuzu dhidi ya Montenegro na Poland zitakazochezwa katiika uwanja wa
Wembley.
Baadhi ya mechi ambayo walisema ilikosa
msisimuko na ambayo ilichezwa mbela ya mashabiki 70,000, meneja huyo wa
England alisema, "kabla ya mchezo, hisia waliyokuwa nayo wengi ni kwamba
matokeo ya sare yoyote hayatakuwa mabaya.''
England iliingia kwenye mchezo huo, bila ya
wachezaji, Danny Welbeck ambaye huchezea Man U , Wayne Rooney na
mshambulizi wa Liverpool Daniel Sturridge ambao hawakucheza kutokana na
majeraha.
Uwezo wetu wa kushambulia ulikuwa mdogo sana kwa sababu hatukuwa na wachezaji, Rooney, Welbeck na Sturridge, alisema Hodgson.
"pia tulimpoteza kiungo cha kati, Alex
Oxlade-Chamberlain kwa sababu ya jeraha la goti ingawa wachezaji
waliowakilisha kwenye mchezo huo walicheza vyema.
Sare hiyo iliisongesha England mbele kwa pointi moja kwenye kundi la H ikisalia na michuano miwili.
No comments:
Post a Comment