RAY C SASA ALITAMANI PENZI LA MKENYA ALIYEOKOA MAMIA YA MATEKA WA AL-SHABAAB KWENYE JENGO LA WESTGATE...!!
Abdul Haji ni miongoni mwa mashujaa
ambao hawatasahaulika nchini Kenya kutokana na kuamua kuhatarisha maisha
yao ili kuokoa watu waliokuwa wamekwama ndani ya jengo la Westagate
baada ya kushambuliwa na Al-Shabaab Jumamosi iliyopita.
Tangu asimulie namna alivyopambana na
magaidi hao, Haji ametokea kuwa kipenzi cha watu wengi hasa wasichana na
mmoja wa watu aliowagusa ni Rehema Chalamila ambaye amesema anatamani
mwanaume mjasiri kama yeye ambaye watazaa naye watoto.
“In love with ths Soldier!i want a
soldier like him to marry me,” ameandika Ray C kwenye picha ya gazeti
aliyoipost kwenye Instagram ikimuonesha Abdul Haji.
“I love You Abdul Haji,You are my Heroooooooo,” aliandika Ray C kwenye picha nyingine.
Kwenye picha nyingine Ray C aliongeza, “My soldier,My Prince,My Love….Love You Abdul Haji.”
Kijana huyo ni mtoto wa waziri wa zamani
wa ulinzi nchini Kenya ambaye alienda kwenye mall hiyo baada ya kupata
ujumbe kutoka kwa rafiki yake kuwa kaka yake alikuwa ndani ya Westgate
wakati watu hao wenye silaha walipovamia.
Akiongea na NTV, Haji ambaye sio
mwanajeshi, alisema alifundishwa kutumia bunduki na baba yake ili
kulinda mifugo yao isiibiwe na wezi.
Ujuzi huo ulimsaidia Jumamosi hiyo
kuwasaidia wafanyakazi wa Red Cross wafanye kazi yao kwa usalama kwa saa
tatu na kusaidia kuokolewa kwa watu wafikao 1,000 nje ya mall hiyo.
No comments:
Post a Comment