PETE YA NDOA IMENIPONZA....NDOA IPO HATARINI.
Wadau nipo njia panda naombeni ushauri wenu, nimefanya kosa kubwa na nalijutia Tafadhali naomba ushauri badala ya kunituhumu.
nilikuta
na demu mmoja tulisoma naye chuo kitambo alikuwa demu wangu for time
being, so baada ya miaka kadhaa tukaja kukuta sehemu, shetani akanipitia
nikavunja amri ya sita naye.
Baada ya kurudi home nikagundua sina pete, nikajaribu kukumbuka nilipoiweka sikupata majibu.
Baada
ya siku kadhaa yule demu akzidi kunisumbua na kutaka niwe karibu naye
sana lakini nikaona si vyema maana anaweza kusababisha mtafaruku kwa
ndoa yangu
Baada
ya kuona nampotezea akaniambia sasa unajifanya mjanja pete yako ni nayo
na nahitaji sh 500,000 cash ama sivyo naharibu kwa mkeo kwamba pete
ninayo na ulinikopa.
Kibaya
zaidi wife aliniuliza pete umepeleka wapi nikadanganya nimeisahau
ofisini nilikuwa nafungua printer sasa pete ikawa inani disturb nikaivua
, nilipoenda jumatatu nikamwambia nahisi wahudumu wa usafi wameiiba
maana siiona pale nimeiweka naendelea na uchunguzi.
Mwanzo
nilimpuuzia lakini mshenzi yule kapeleleza hadi wife anapofanya kazi na
kapata simu yake, juzi kampigia kamwambia "naomba mkumbushie mumeo deni
langu mimi xxxxx nampigia simpati" halafu akakata simu.
Niliporudi
wife kanibana nikamwambia ni mambo ya kazi tu akataka kujua no yake
kaipataje, nikazuga zuga na ubabe wa kiume yakaisha
Nikipiga akili nimuendee Polisi naona kama kitanuka na wife atajua
Nikifikiria kumlipa akili hainipi kabisa....kilo tano?
Sijui nimueleze wife ukweli?
Nimejaribu kumpigia simu na kumbembeleza kagoma anachohitaji ni kilo tano au aniharibie kwa wife.
Tafadhali ushauri wakuu lawama na madongo hayatanisaidia.
No comments:
Post a Comment