Mwanamke mwenye mimba bandia na Cocaine

Raia wengi wa kigeni wamenaswa nchini Colombia mwaka huu wakiwa na dawa za kulevya

Raia mmoja wa Canada amekamatwa nchini Colombia baada ya kujaribu kupanda ndege kurejea Canada akiwa na tumbo bandia ya ujauzito alimokuwa ameficha dawa ya kulevya aina ya Cocaine.

Mwanamke huyo aliyekuwa anajifanya kuwa mtalii akirejea Toronto, alihojiwa na polisi katika uwanjwa wa ndege wa Bogota aliyemshuku na kumuuliza alikuwa amesalia na miezi mingapi kujifungua.

Afisaa huyo aligusa tumbo lake na kuhisi ilikuwa baridi mno na ngumu sana ndiposa wakaamua kumkagua zaidi.

walimpata na dawa za kulevya zilizokuwa zimefungwa ndani ya tumbo bandia ya mimba ambayo mwanamke huyo alikuwa ameivaa kwa kufunga tumboni.

Inasemekana kuwa alisema ana miezi saba ya ujauzito lakini baada ya polisi kumkagua walimpata na Cocaine kilo mbili iliyokuwa ndani ya vipochi viwili

Mwanamke huyo atashtakiwa kwa kosa la ulanguzi wa madawa ya kulevya na huenda akafungwa jela kwa miaka mitano au nane.

Mwaka huu pekee karibu watu 150 wamekamatwa na madawa ya kulevya katika uwanja wa ndege wa Bogota.

Karibu thuluthi moja ya waliokamatwa walikuwa raia wa kigeni, kwa mujibu wa maafisa wakuu nchini Colombia.

No comments: