Lionel Messi alipa kodi aliyokwepa
Lionel Messi
Lionel Messi -nyota ya Barcelona
na timu ya Taifa ya Argentina pamoja na babake wamelipa euro milioni
tano(sawa na dola milioni 6.6) deni la kodi kabla ya kukabiliana na
mashtaka ya kukwepa kodi kwa njia za ujanja, kwa mujibu wa uwamuzi wa
jaji mapema leo Alhamisi.
Madai haya ya kukwepa kodi yaliyowasilishwa
mahakamani mapema mwezi juni yalikua pigo kubwa kwa hadhi ya mcheza soka
huyu ambaye kabla ya hapo alionekana kama mnyenyekevu asiye mizengwe
ukimlinganisha na mtani wake mkuu Cristiano Ronaldo mwenye mbwembwe.
Maamuzi ya jaji huko Gava, kwenye
pwani ya bahari Mediterenian karibu na mji wa Barcelona, amesema kua
babake Messi Jorge Messi alilipa euro milioni 5.02 kwenye mahakama
tarehe 14 mwezi Agosti kufidia kodi inayodaiwa haikulipwa pamoja na
riba.
Jaji huyo amepinga ombi la mwanasheria wa
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutaka alipe kwa dhamana ya hisa
ili kuhakikisha kua riba yoyote itakayosababishwa na kesi inalipwa.
Jaji alisema kua haina haja kwa sababu ya uwezo
alio nao Bw.Lionel Andres Messi Cuccittini akiongezea kua tayari kodi
hiyo imeisha lipwa.
Suala ambalo jaji huyo amesema bado anashauriana
na mwanasheria wa upande wa mashtaka ni kuhusu ombi la Messi kutaka
kusikilizwa kwa kesi hiyo kuahirishwe kutoka tarehe 17 septemba.
Mashtaka dhidi ya Messi na babake Jorge ni
kuhusu kuibia kodi inayotokana na mapato ya biashara zinazotumia sura
yake kuanzia mwaka 2006 na 2009.
Inadaiwa kua Messi na babake walijaribu
kulihadaa taifa kwa kuhamisha hati miliki za malipo hayo kwenye
makampuni yaliyo nje kama huko Belize na Uruguay ili wasilipe kodi
nchini Uhispania.
Mawakili wa Messi Juarez Veciana, wamesema kua
mteja wao anakubaliana na sheria za Uhispania na yupo tayari kulipa kila
fedha anayotakiwa kulipa.
Ufanisi wa Messi uwanjani umemfanya kua mmoja ya
sura zinazouzika duniani akiwa namba 10 kwenye orodha ya Forbes
miongoni mwa wana michezo mashuhuri wenye mapato makubwa akikadiriwa
kupokea dola milioni 21 kila mwaka kutokana na matangazo ya biashara
peke yake.
No comments:
Post a Comment