England haitashinda kombe la dunia'
Greg Dyke
Mwenyekiti wa chama cha soka
nchini Uingereza Greg Dyke, amesema kuwa hana matumaini ya Uingereza
kushinda kombe la dunia nchini Brazil mwaka ujao.
Akiwahutubia waandishi wa habari mjini London,
alitaka timu ya Uingereza kujitahidi kufika nusu fainali ya kombe la
Uropa mwaka 2020 na kuwa na matumaini ya kushinda kombe la dunia mwaka
2022.
Aliambia BBC kuwa: "haimaanishi kuwa hawawezi kufanya vyema nchini Brazil, muhimu wafuzu tu.''
"sidhani kama hata tunaweza kushinda kombe la dunia nchini Brazil.''
Uingereza wanakabiliwa na kibarua kigumu katika
siku chache zijazo wakati watakapojaribu kufuzu kushiriki michuano ya
kombe la dunia nchini Brazil mwaka ujao.
Kikosi cha kocha Roy Hodgson, waliobanduliwa nje
ya michuano ya robo fainali ya mataifa ya Ulaya mwaka 2012, watacheza
na Moldova katika uwanja wa Wembley siku ya Ijumaa. Waliicharaza timu
hiyo mwaka jana mabao matano bila, baadaye Jumanne watasafiri kwenda
Ukrain
Kwa sasa wanashikilia nafasi ya pili kwenye
kundi H, alama mbili nyuma ya Montenegro, ambao wamecheza mechi moja
zaidi ya Uingereza.
Hata hivyo Dyke ana matumaini makubwa kuwa
England itafuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia Brazil. Wakati wa
mwisho kwa England kushinda kombe la dunia ilikuwa mwaka 1966.
No comments:
Post a Comment