Jeshi la Nigeria lawaua wapiganaji 150
Wanajeshi 9 wangali hawajulikani waliko baada ya makabiliano makali kuzuka kati ya wapiganaji na wanajeshi hao mjini Borno
Jeshi la Nigeria, linasema kuwa
limewaua wapiganaji 150 wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko
Haram wakati wa msako dhidi yao wiki jana.
Makabiliano yalitokea wakati jeshi lilipokuwa
linafanya msako dhidi ya wapiganaji hao katika jimbo la Borno Kaskazini
Mashariki mwa nchi.
Katika taarifa yake, jeshi lilisema
kuwa takriban wanajeshi 16, walifariki wakati walipofanya shambulizi la
kwanza dhidi ya kambi ya wanajeshi hao ambako walipata silaha nzito
Wanajeshi wengine wa serikali wanasemekana
kutojulikana waliko. Aidha jeshi lilisema pia liliweza kumuua kamanda wa
wapiganaji hao Abba Goroma.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa,
jeshi kwa kawaida huongeza chumvi idadi ya wapiganaji waliouawa kwa
lengo la kuonyesha kuwa wanajeshi waliouawa kwenye mapigano walikuwa
wachache.
Boko Haram ilianza harakati zake mwaka 2009 katika jimbo la Borno ambalo hadi sasa liko chini ya sheria ya hali ya hatari.
No comments:
Post a Comment