Cash Money Wako Tayari Kumtoa Upya Msanii Huyu

Msaani mpya wa Cash Money aliye leta gumzo sana baada ya kupewa mkataba wa kurekodi ametangaza tarehe ya kutoka kwa wimbo wake wa kwanza kama msanii wa Cash Money. Paris Hilton ametangaza wimbo wake utatoka October 1 2013, Utaitwa Good Time na kashirikishwa rapper Lil Wayne. Mpaka sasa audio na video ya wimbo huu vimefanyika na viko tayari kutoka mwezi wa kumi.

November Mwaka jana Paris Hilton alitoa wimbo Last Night ft lil wayne na Mwaka huu mwezi wa tano, May 2013 Hilton alipata mkataba chini ya Cash Money na August alipanda kwenye jukwa moja na Lil Wayne na kuimba nane kwenye Birthday yake.

Album ya mwisho ya Paris Hilton ilitwa Paris ilitoka mwaka 2006, na kushirikisha wasanii kama Fat Joe na Jadakiss.

No comments: