Bensouda:'Ruto alimiliki jeshi la kivita'
Bwana Ruto na wafuasi wake alipokuwa anaondoka Kenya kuelekea Hague
Naibu rais wa Kenya William Ruto
amekana mashitaka ya uhalifu katika kesi inayoendeshwa kwenye mahakama
ya kimataifa ya uhalifu ICC , Hague Uholanzi.
Bwana Ruto -- ambaye anatuhumiwa kupanga ghasia
za baada ya uchaguzi uliokuwa na utata wa mwaka 2007 -- amekana mashtaka
hayo sawa na mshitakiwa mwenza katika kesi hiyo mtangazaji Joshua Arap
Sang.
Mwendesha mkuu wa mashtaka katika
ICC, Fatou Bensouda, alimtaja Ruto kuwa mwanasiasa shupavu ambaye
alipanga kufanya uhalifu dhidi ya binadamu ili kujinufaisha kisiasa.
Amesema kuwa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka
2007, Ruto aliunda jeshi lake la kivita kumpigania dhidi ya mahasimu
wake madai ambayo yamekanushwa na wakili wa Ruto bwana Khan
Bwana Ruto na Rais Uhuru Kenyatta pamoja na
mwandishi wa habari Joshua Arap Sang, wanatuhumiwa kwa kuhusika na
ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, kufanya mauaji kuchochea na
kupanga ghasia hizo.
Rais Uhuru Kenyatta ambaye pia anatuhumiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu, anatarajiwa kufikia katika mahakama hiyo mwezi Novemba
No comments:
Post a Comment