Baby Madaha nomaaa!! Asaini mkataba wa shillingi millioni 50 na yule Meneja wa Mr. Nice Kenya; apewa na Audi ya kutembelea..Soma hapa
Baby
Madaha nomaaa!! Asaini mkataba wa shillingi millioni 50 na yule Meneja
wa Mr. Nice Kenya; apewa na Audi ya kutembelea..Soma hapa
Mwanadada anayefanya vizuri sana kwenye muziki na filamu,baby
Madaha amelamba bingo ya uhakika na kampuni ya Candy n’ Candy Records
Label ya jijini Nairobi iliyomsainisha mkataba msanii mwingine wa
Tanzania Mr.Nice hivi karibuni.
Akizungumza kwa simu na bongomovies leo meneja wa msanii huyo
Joe Kariuki amesema kuwa pamoja na msanii huyo kupewa mkataba huo wa
million hamsini (50) pia wamempa mwanadada huyo gari ya kutembelea ya
kisasa aina ya AUDI TT (pichani) na nyumba kali mitaa kijitonyama jijini Dar es salaam.
Pamoja na hayo pedeshee huyo wa Mr.Nice ambaye ndio mmiliki wa
studio hiyo amesema wanataka kumuhamishia msanii huyo jijini Nairobi
nchini Kenya kwa kipindi cha mwaka mmoja ili afanye nao kazi huko kwani
wamegundua kuwa anakubalika sana nchini humo na wapenzi wa muziki.
Baby madaha ambaye anatarajia kutua nchini leo akitoka Nairobi
pamoja na meneja wake kwa ajili ya kuachia video ya wimbo wake wa
kwanza aliofanya na Label hiyo uitwao (Summer Holiday) ambao umefanywa
huko huko jijini Nairobi