BABY MADAHA ANASWA LIVE NA MUME WA MTU.....!!
STAA wa sinema na Bongo Fleva, Baby Madaha amenaswa live akiingia na
kula bata hotelini akiwa na mwanaume aliyetajwa kwa jina la Joe Kariuki.
Tukio
hilo lililopigwa chabo na shushushu wetu lilijiri wikiendi iliyopita,
majira ya usiku mnene katika Hoteli ya De France iliyopo Sinza, Dar
ambapo Madaha alionekana akiwa amejiachia vya kutosha kwa mwanaume huyo.
Ili
kupata mzani wa habari hiyo, gazeti hili lilizungumza na Madaha ambaye
alikiri kuwa na mwanaume huyo hotelini hapo huku akidai ni meneja wake.
“Joe
(Kariuki) ni meneja wangu wa Kampuni ya Candy n’ Candy Records ya
Nairobi, Kenya ndiye anayesimamia kazi zangu na tayari nimeachia ngoma
moja inayo-hit ya Summer Holiday,” alijitetea Madaha.
No comments:
Post a Comment