SINTAH YAMKUTA-HABARI YA UONGO ALIYOIANDIKA NA KUIWEKA KWENYE BLOG YAKE YAMTOKEA PUANI POLISI WAANZA KUMFUATILIA..
Msanii zilipendwa kwenye sanaa ya filamu Sintah amefanya madudu mengine
baada ya kuandika habari ya uongozi na uchochezi na kukipakazia kituo
cha redio time fm cha Jijini Dar kuwa kilishindwa kujipanga kwenye shoo
yao iliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye suala la ulinzi hadi kupelekea
wasichana kubakwa na kuporwa mali zao.
Habari hiyo iliwashangaza waandaji wa tamasha hilo pamoja na jeshi la
polisi Kanda ya Kinondoni ambalo lilikuwepo uwanjani usiku kucha
wakingozwa na mkuu wa kituo cha Polisi Oysterbay Wilbrod Mtafungwa hadi
asubuhi bila kushuhudia matukio mabaya.
Katika habari hiyo ya Sintah iliyokuwa inasema kuwa Wasichana wabakwa
usiku kucha na wahuni kwenye shoo ya Azonto bila msadaa wowote jambo
ambalo Jeshi la Polisi Kinondoni limekanusha vikali madai hayo huku
ikisema kuwa hadi leo Jumanne hakuna taarifa yoyote kuhusiana na madai
hayo ya Sintah.
Akiongea mmoja wa askari wa kituo cha Oysterbay ambae aligoma kutaja
jina lake kwa madai kuwa yeye si msemaji alisema" Tumeshangazwa sana na
taarifa ya Sintah aliyoiandika jana Jumatatu mapema kuwa kuna wasichana
walibakwa usiku kucha hii habari naona ilikuwa na mlengwa wa kushoto kwa
kuchafuliana habari hiyo haina ukweli wowote kwani hadi sasa sisi kama
Polisi tuliopewa jukumu la kulinda wananchi ziku zile hatuna taarifa
hizo" Alisema afande huyo
Hata hivyo jeshi hilo lilikuwa na mpango wa kuhitaji ushahidi wa
vielelezo juu ya habari hiyo ambavyo Sintah angetakiwa kuviwakilisha
polisi ili waweze kuwasaka wabakaji hao vinginevyo habari hiyo
ingemletea matatizo Sintah kwani ni ya uchochezi na unafiki.
Siku ya shoo hiyo ya mwanamuziki Azonto toka nchini Ghana
mwenye makazi yake nchini Uingereza ilikuwa na ulinzi mkali sana
kulikuwa na Mbwa wa polisi 15, Polisi wasiopungua 90 wakiwemo wale wenye
siraha ambao walikuwa wanazunguka viunga vya uwanja wa Ustawi wa Jamii.
Aidha baadhi ya mashabiki wengi walisema kuwa huenda Sintah bado ana
hasira na kituo hicho cha redio times baada ya kupigwa chini kwenye
kipindi alichokuwa anatangaza kutokana na kukosa sifa ya kuendesha
kipindi hali iliyosababisha Sintah kuwawekea bifu.
Hata hivyo Sintah aliitoa haraka habari hiyo kwenye blog hiyo baada ya
kutonywa na wasamalia wema kuwa ingemletea matatizo makubwa kwani kama
hana ushahidi wa vielelezo ni heri akaitoa na mara moja alifanya hivyo.
Xdeejayz iliwasiliana na uongozi wa redio times lakini bahati mbaya simu
zao zote zilikuwa bize kila walipopigiwa simu, hata hivyo tunawaahidi
wasomaji wetu kuwa itamtafuta mkurugenzi wa kituo hivho Rehure Nyaulawa
kuzungumzia suala hilo na kama kuna hatua zozote wameshaanza kuzichukua
juu ya Blog hiyo kwa kuandika habari hiyo ya uongo.