PATA HABARI KWA UFASAHA HAPA
e-mail; edonisaya@gmail.com
e-mail; edonnathanael@yahoo.com
twitter; Edon Isaya
facebook; Edon Isaya
phone; 0654894210
phone; 0682426975
www.edonisaya.com
JOKETI ATOA SOMO KWA WANAWAKE WAPENDA PESA.PIA ATOA SABABU ZA YEYE KUPENDWA NA WANAUME.
MREMBO
anayefanya vizuri katika mambo mengi nchini, Jokate Urban Mwegelo
(pichani) ametaja sababu nne zinazowafanya wanaume kumzimikia, akiwemo
nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akiandika
katika mtandao wake wa Kidoti Life Style, Jokate, mshindi wa pili wa
Miss Tanzania 2006, alizitaja sababu hizo kuwa ni kujiamini,
kujitegemea, kupendeza na tabasamu muda wote.
“Kujiamini
ndiyo sababu kubwa ya kwanza inayonifanya nipendwe zaidi, hamna kitu
kinachowavutia watu hasa wanaume kama kujiamini,” anaandika Jokate.
“Kujitegemea
ni sababu ya pili, binafsi naamini kwamba hakuna kitu kinachowaboa
wanaume kama mwanamke ambaye anapenda vitu vya kupewa. Ukimuonesha
mwanaume wewe unapenda kutafuta vyako, basi jua atakupenda zaidi.”
Jokate
alisema sababu nyingine inayomfanya kuwa kivutio kwa wanaume ni
kupendeza katika mavazi, hasa kwa kuvaa nguo zenye rangi ya kuonekana.
Sababu nyingine aliyoitoa ni tabasamu, akiweka wazi kuwa tabasamu linamfanya aonekane mrembo zaidi.
No comments:
Post a Comment