MWENYEKITI
wa Kamati ya Umoja wa Mashirikisho ya Sanaa Tanzania, Kimela Billa,
ameutaka uongozi wa Shirikisho la Muziki Tanzania, kumchukulia hatua ya
kinidhamu, msanii wa muziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa kosa
la kukiuka maadili ya Tanzania katika tamasha la Serengeti Fiesta,
mkoani Iringa.
Shilole
alipanda jukwaani akiwa anacheza wimbo wake wa ‘Nakomaa na jiji’ huku
akiwa amevaa nguo ambazo zinaonesha maumbile yake yote ya mwili.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Billa alisema Shirikisho la muziki chini ya rais
wake, Addo Novemba wanatakiwa kuchukua hatua zaidi juu ya shilole kwa
kosa la kuwadhalilisha wanawake ikiwa ni pamoja na kukiuka maadili ya
Tanzania.
“Hatukatai
hayo mambo yapo lakini kwa staili ile sisi kama viongozi wa sanaa
hatutaweza kuvumilia, shirikisho la muziki wakishindwa kutekeleza hili
lazima kamati ilivalie njuga swala hilo, kiukweli wanalidhalilisha taifa
hawa wasanii, mbona wanaume hawafanyi shoo zao uchi,? Alihoji Billa.
Alisema
shirikisho la muziki liige mfano wa shirikisho la filamu kama
lilivowaonya Wema Sepetu na Aunt Ezekiel kwa makosa kama hayo, ambapo
anamini kwaasilimia kubwa kunachangia kuwa na nidhamu wanapopanda
jukwaani.
SHILOLE AFANYA KUFURU FIESTA, BIKINI ,SHANGA VYOTE NJE NJE STAILI ZA NGONO ZATAWALA