Huenda Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae Zanzibar,
Anselmo Mwang’amba aliyemwagiwa tindikali siku tano zilizopita,
akasafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu kutokana na Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili ambako amelazwa, kudaiwa kushindwa kumtibu.
Akizungumza na gazeti hili jana, padri huyo
alisema anategemea kwenda nje ya nchi kwa matibabu japokuwa bado hajajua
nchi atakayopelekwa kwa kuwa anasubiri ushauri wa madaktari.
Alisema pamoja na matibabu aliyoyapata lakini bado anasikia maumivu katika majeraha ya usoni, mikononi na kifuani.
Aliisihi Serikali kukomesha na kuwakamata wahusika
wa vitendo hivyo vilivyokithiri vya kuwamwagiwa watu tindikali bila
sababu visiwani humo.
Hata hivyo, habari zilizopatikana kutoka katika
chanzo kilichopo ndani ya hospitali hiyo kimeeleza kuwa, padri huyo
anatarajia kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu kwani inadaiwa majeraha
yake yameshindikana kutibiwa nchini, japokuwa bado haijajulikana ni nchi
gani atakayoenda kati ya mbili zinazotajwa na viongozi hao, Afrika
Kusini na India.
Alisema madaktari wataalamu waliopo katika
hospitali hiyo wana uwezo wa kumponya Padri huyo lakini tatizo lililopo
ni ukosefu wa vifaa vya kisasa ndiyo maana wagonjwa wengi wanaomwagiwa
tindikali hupelekwa kutibiwa
No comments:
Post a Comment