MWANAMKE ADAIWA NDIO KIONGOZI WA MAGAIDI WA AL SHABAAB WALIOTEKA WESTGATE MALL KENYA.
Mwanamke
raia wa Uingereza, Samantha Lewthwaite aka The White Widow, *anahisiwa*
kuongoza kundi la magaidi wa Al-Shabaab walioivamia mall maarufu ya
Westgate ya jijini Nairobi nchini Kenya jana na kuwaua watu zaidi ya 68
na kujeruhi wengine zaidi ya 175.
Tayari
mashirika makubwa ya habari duniani yakiwemo, CNN, The Sun na IBTimes
yameandika habari kuhusu uwezekano wa mwanamke huyo kuwa kiongozi wa
magaidi hao walioshambulia Westgate.
Nayo
akaunti ya Twitter ya American Jihad Watch @watcherone, imepost picha
ya gaidi wa kike iliyedai ilipigwa na camera za ndani ya mall huyo na
kudai kuwa ‘huenda’ akawa ni The White Widow. “Female jihadi caught on
mall camera at Westgate Centre Shopping mall earlier yesterday may be
infamous ‘White Widow’, imesomeka tweet hiyo.
Picha ya gaidi akiwa ndani mall hiyo
Kwa mujibu wa baadhi ya watu waliokolewa kwenye mall hiyo, miongoni mwa magaidi hao alikuwepo mwanamke wa kizungu.
Kwa
mujibu wa CNN, magaidi watatu ni wa Marekani, mmoja wa Kenya,
Uingereza, Finland na wawili wa Somalia. Bado wamo ndani ya mall hiyo.
Hata
hivyo Kwa mujibu wa mtandao wa Telegraph, jana usiku ofisa wa shirika
la kupambana na ugaidi Kenya alikanusha taarifa kuwa Samantha Lewthwaite
anaweza kuhusika na shambulio la jana.
Samantha Lewthwaite aka The White Widow ni nani?
Ni
mwanamke anayetafutwa kwa udi na uvumba kwa kuhusika kwake kwenye
matukio mbalimbali ya kigaidi nchini Uingereza na Afrika Mashariki. Yeye
ndiye aliyepanga shambulio la kigaidi jijini London la mwaka 2005
lililosababisha vifo vya watu 52 ambapo mume wake Jermaine Lindsay
alijitoa muhanga.
Akitokea
Aylesbury, Buckinghamshire, nchini Uingereza, The White Widow kwa sasa
ni kiongozi wa juu wa mashambulio ya Al Shabaab nchini Kenya na Somalia.
Mwanamke huyo anadaiwa kuwa mfadhili mkuu wa shughuli za kundi hilo la
kigaidi.
No comments:
Post a Comment