MWAKYEMBE ABAINI KUTOBOLEWA KWA BOMBA LA MAFUTA BANDARINI..ATOA SIKU MBILI.
Waziri
wa uchukuzi Dkt. Harrisoni Mwakyembe amebaini wizi wa mafuta katika
bomba la mafuta mjimwema na kuagiza maskari wa usimamizi wa bandari
Tanzania kuwakilisha majina ya wahusika ndani ya siku mbili.
Mwakyembe
ameyasema hayo wakati akizungumza na wafanyakazi wa mamlaka ya
usimamizi wa bandari Tanzania (TPA) na kulaani kitendo cha baadhi ya
watu kutoboa bomba hilo na kuunganishia mabomba yao madogo na kuyafungia
kwenye maputo yenye uwezo wa kubeba mafuta kati ya lita 16-18 kinyume
cha sheria na kukiita kitendo hicho ni kuhujumu uchumi wa nchi ambapo
ameishutumu kampani ya ulinzi ya tipa kuhusika na kitendo hicho na
kuwataka kumpa picha za wafanyakazi wote waliokuwa kitengo cha ulinzi na
kama hawatafanya hivyo kampuni hiyo italipishwa fidia.
Naye
kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania
Mhandisi Madeni Kipande wakati akijibu mapendekezo yaliyotolewa na
waziri mwakyembe kuhusu wafanyakazi wa mamalaka hiyo amesema kuwa
wafanyakazi waliokuwa wameajiriwa kama vibarua watapewa ajira za kudumu
na kubainisha kuongezewa posho wafanyakazi hao kutoka laki moja awali na
kufikia laki mbili pamoja na laki moja na nusu kama ghrama za chakula
No comments:
Post a Comment