MDOSI
au Kanjibai aliyefahamika kwa jina moja la Milah ambaye ni bosi wa
kampuni moja ya ujenzi yenye makao yake Mwenge jijini Dar alinaswa
chooni akiwa na mfanyakazi wake, John Carlos ‘Shabani’ (watu
walimpachika jina la Shabani kutokana na Kanjibai wa kwenye Komedi)
ikidaiwa walikuwa katika mazingira ya ulawiti...
Ishu
hiyo nzito ilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo wawili hao
walikuwa chooni humo kwa zaidi ya nusu saa na kuwasababishia usumbufu
watu waliokuwa wakitaka kutumia choo hicho.
KISA KILIPOANZA
Siku
hiyo ya tukio, mtu mwenye sauti ya kiume alipiga simu kwenye chumba cha
habari , Mwenge jijini Dar na kupasha juu ya tukio hilo. Alisema:
Mtoa habari huyo alikwenda mbele zaidi kwa kuwaambiwa waandishi wetu waliompokelea simu wachukue Bajaj au Bodaboda ili kuwahi.
Sosi
huyo kabla ya kukata simu aliweka wazi ramani ya kufika kwenye choo
hicho na kusisitiza kwamba muhimu kuwahi kwa sababu huenda wanagombana.
Kufuatia
msisitizo huo, waandishi wetu makini waliwasha pikipiki zao, kila
mmoja na yake na kushika njia kuelekea eneo la tukio.
Hata
hivyo, kwa kuamini wanaweza kukutana na lolote, waliona ni vyema kwanza
kwenda kutoa taarifa kwenye Kituo Kidogo cha Polisi cha Mwenge ambapo
walipewa askari wawili kuelekea eneo la tukio.
ENEO LA TUKIO SASA
Timu
hiyo iliwasili kwenye eneo la tukio. Mlango wa choo hicho ulikuwa
umefungwa lakini kwa mara moja tu haikuwa rahisi kugundua kama ulifungwa
kwa funguo au kawaida tu.
Afande mmoja alijitolea kugonga mlango wa choo hicho ili kupima ushirikiano utakaotolewa na wawili hao au mmoja wao.
Sauti iliyoonekana ni ya Kanjibai kutokana na kushindwa unyoofu wa lugha ya Kiswahili ilisikika ikiuliza:
“Nani wewee… taka nini huku?”
Afande: Sisi ni askari polisi, fungua haraka tunajua mko wawili humo ndani, fungua.
Kanjibai: Subiri kidogo.
Baada ya dakika kadhaa , mdosi huyo alifungua mlango na kukutwa akiwa na ‘Shabani’.
WALICHOKUWA WAKIKIFANYA CHOONI
Katika
maswali ya harakaharaka nje ya choo hicho kila mmoja alisema la kwake
ambalo aliliamini linaweza kumchomoa kwenye skendo hiyo mbaya.
‘Shabani’
alisema yeye aliingia kwenye choo hicho baada ya kuitwa na bosi wake
huyo ambapo alishindwa kumkatalia kwa kuogopa kupoteza ajira yake na
kama inavyojulikana maisha ya Dar bila kazi ni ngumu kuyamudu.
Alipoulizwa walichokuwa wakikifanya ndani ya choo hicho, Shabani alibaki akiwatumbulia macho maafande.
Kwa
upande wake Kanjibai alipotakiwa kujieleza kisa cha kuingia chooni na
mfanyakazi wake, alisema alimuomba wazame humo ili akamnyoe. Yaani
Kanjibai alitaka kunyolewa.
IKAFIKA ZAMU YA KUPELEKWA KITUONI
Afande
mmoja aliamuru wawili hao wapelekwe kituo cha polisi, lakini kabla ya
kuanza safari, mdosi huyo aliingiza mkono kwenye mfuko wa suruali na
kutoa vitu vyake kadhaa na kuwakabidhi wadosi wenzake waliofika
‘kumsaidia’ muda mfupi baada ya kunaswa.
Halafu
aliingiza mkono kwenye mfuko mwingine na kutoa mafuta aina ya KY ambayo
mtaani hujulikana sana kwa jina la ‘mlainisho’ lakini askari alimwambia
mafuta hayo yanatakiwa kituoni kwa ajili ya ushahidi hivyo asiwape
nduguze.
Breki
ya kwanza ilikuwa kwenye Kituo Kidogo cha Polisi Mwenge ambapo baada ya
mahojiano mafupi walihamishiwa Kituo cha Polisi cha Kijitonyama
‘Mabatini’ ambapo walihojiwa zaidi kuhusiana na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment