MAJANGA MENGINE KWA HUYU MSANII WA FILAMU ZA BONGO NI HAYA HAPA!!
BINAFSI
nafahamu kwamba Irene Uwoya aliwahi kuwa staa mkubwa nchini lakini
akafanya makosa na sasa ameshuka chati. Ameporomoka kwa kiasi kikubwa
sana.
Elizabeth
Michael ‘Lulu’, baada ya ‘ajali’ yake na marehemu Steven Kanumba,
alikaa mahabusu kwa zaidi ya mwaka mmoja lakini baada ya kutoka
ameonekana kuwa na mafanikio makubwa kuliko Uwoya ambaye siku zote yupo
mtaani.
Pengine
kuna aina fulani ya maisha ambayo Uwoya amejichagulia maana akina Rose
Ndauka, Aunt Ezekiel, Wema Sepetu na wengineo wamekuwa wakifanya vizuri,
wanamfunika sana. Ameshindwa kujisahihisha, ataendelea kusugua.
Najua
kwamba Uwoya ana hali mbaya kisanii, amechoka, muonekano wake
hausisimui tena, amepoteza mashabiki, kwa maana hiyo hauzi. Dili za
kucheza filamu zinaota mbawa kila kukicha, maprodyuza wanataka wakali
ambao wanafanya biashara sokoni.
Naelewa
kuwa hivi sasa katika ulimwengu wa masupastaa, Uwoya amebaki
msindikizaji lakini sikuwahi kufikiri kwamba anaweza kufikia hatua mbaya
kiasi hicho. Kafikishwa mbaroni kwa wizi wa simu? Yaani wizi wa simu ya
mkononi! Anatia huruma.
Yamemfika
yapi? Sitaki kuamini kama Uwoya anashindwa kununua simu halali. Akili
nyingine inaniambia kuwa hawa dada zetu wanaharibiwa na uchu wa kupenda
vitu vya juu lakini uwezo ni mdogo. Je, huo wizi wenyewe alifanyaje?
Atakapofikishwa
mahakamani pengine itajulikana kama kweli amehusika na wizi huo, basi
itafahamika ameufanyaje. Ni yeye moja kwa moja au kupitia kwa mtu
mwingine? Dunia ina mengi, ni vizuri hili jambo likafika kortini, huko
tutajua ukweli halisi.
Swali langu ni hili, kama kweli ile simu
alinunua kwa nini pale kituoni hakutoa risiti? Hata kama ingekuwa
nyumbani, alishindwa nini kuagiza aletewe kuthibitisha kama ni mali
yake? Maswali hayo mawili yanaongeza uzani kwenye madai kwamba ile simu
ni ya wizi.
Ni ya wizi sawa, je, ni kweli Uwoya anaweza kuiba simu?
Inawezekana kabisa akatega Kariakoo halafu amvizie mtu na kumchomolea?
Maana mashtaka dhidi yake ni Wizi wa Maungoni, yaani wizi wa kumchomolea
mtu kitu kutoka mwilini.
Kesi ipo Msimbazi Polisi na imeandikwa
kwenye kitabu cha ripoti za kumbukumbu (report book ‘RB’) kwa nambari
MS/RB/8522/2013. Hata hivyo, simu yenyewe iliyoibwa ina thamani kubwa,
nahisi Uwoya aliinunua kwa mtu ambaye ndiye mwizi.
Mikono ya Uwoya na
vidole vyake vilivyo, haoneshi kama anaweza kuwa mkali wa kuchomolea
watu. Hata kama kaishiwa na kupigika, siyo rahisi akafanya hivyo. Sura
yake haioneshi ushujaa wa ‘kupiga ndole’ lakini ya Mungu mengi.
Labda
kauziwa lakini yeye ndiye kakutwa na mali ya wizi (aliyekutwa na ngozi
ndiye aliyeiba ng’ombe). Kama ipo hivyo, hilo nalo ni tatizo kubwa.
Maana yake yeye naye ni mmoja wa watu wanaowafanya wezi waendelee
kufanya uporaji. Anawafadhili kwa mlango wa nyuma.
Tusimamie hapa
kwamba kama alinunua, basi Uwoya ni mfadhili wa wezi kwa sababu mtu
anayenunua mali ya wizi, anawasaidia wezi kuendelea kuishi kwa uporaji.
Kwa maana hiyo siyo mtu mzuri, hafai kwenye jamii.
Kwa mwenendo huo,
naamini ndiyo maana ameporomoka, anakosa sifa ya kuitwa kioo cha jamii.
Inawezekanaje awe mfano wa kuigwa ikiwa yeye ni kirusi katika hiyohiyo
jamii? Mtu unajua kabisa hii mali ya wizi unainunua kwa bei chee halafu
unaona raha.
Kununua mali ya wizi ni hujuma nzito, ni ukosefu wa
huruma kwa sababu wakati wewe unauziwa mali hizo kwa bei nafuu sawa na
bure, halafu unaitumia kwa nafasi huku ukijionesha, mwenzako anateseka
mno.
Fikiria kama wewe umejibana, ukajitutumua kununua simu aina ya
iPhone 5 kwa shilingi milioni 1.6. Umeitumia wiki mbili tu unaibiwa,
halafu mtu mwingine anakuja kuuziwa kwa shilingi 400,000 au 300,000.
Itakuuma kiasi gani?
Bila shaka utamchukia mwizi na yule aliyeuziwa,
kwani angekuwa muungwana asingekubali kununua. Laiti angekuwa raia
mwema, angesaidia huyo muuzaji akamatwe ili aliyeibiwa arudishiwe mali
yake. Kutumia mali ya wizi ni dhuluma, ni wizi.
Uwoya alikamatwa na
simu ya wizi aina ya iPhone 5, kwa hiyo kama aliuziwa, na kwa mujibu wa
tafsiri ambayo nimeielezea hapo juu ni wazi kwamba yeye siyo raia mwema.
Ukweli uzidi kusimama kwamba hafai kuitwa kioo cha jamii.
Je, ni
tamaa ya kutaka vitu vizuri wakati pesa hana? Ajioneshe mjini kwamba
anamiliki iPhone 5 kumbe ni ya wizi, ameipata kimagumashi. Namshauri
Uwoya aache mtindo wa kuishi kimagumashi, kama hana akubali hali halisi.
Si kulazimisha maisha ya gharama, matokeo yake ndiyo haya.
ANGEMTII MUMEWE YASINGEMFIKA HAYA
Nikiongoza
jopo la waandishi kutoka Global Publishers Ltd, mwaka jana,
tulifanikisha kumsuluhisha Uwoya na mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’
kutokana na mgogoro wa nguvu ambao ulikuwa unaitikisa ndoa yao.
Malalamiko
ya Kataut yalijikita katika uaminifu, kwamba Uwoya alikuwa anaonesha
alama nyingi kuwa si mwaminifu kwenye ndoa yao. Mume huyo, alisema
kwamba amenunua vifaa na kuanzisha kampuni ili mkewe ajisimamie katika
kazi zake za filamu lakini mke hataki.
“Analipwa pesa kidogo ambayo
akifanya shopping tu zinakwisha, maprodyuza wanapata fedha nyingi, yeye
anafanya kazi, anauza sura tu lakini pesa hakuna. Nataka atengeneze
filamu zake ili apate pesa za kuonekana lakini haelewi wakati kila kitu
nimeshanunua,” Kataut alilalamika.
Kataut alikuwa na nia ya dhati
kabisa ya kumwokoa Uwoya na pengine kama angefuata mwongozo wa mumewe
leo hii asingeporomoka kama alivyo. Pengine yanayomkuta leo ni malipo ya
kile ambacho alimtendea mwanamme huyo.
Mke wa mtu kunaswa hotelini
na kijana wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ni aibu sana! Kabla ya
hapo zilishaibuka stori kwamba amegombana na supastaa Jacqueline Wolper
kisa mwanaume. Alimtesa sana Kataut wa watu.
Akiwa yupo ndani ya
ndoa, akaingia kwenye mgogoro na boyfriend wake wa zamani, Hamis
Ramadhan Baba ‘H-Baba’, akadai eti katika wanaume wake wote waliopita,
ambaye hawezi kurudiana naye ni H-Baba. Huyu ni mke wa mtu.
Tafsiri;
kumbe pamoja na kuwa kwenye ndoa, anaweza kurudiana na wanaume wake wote
waliotangulia isipokuwa tu H-Baba. Je, unamuonaje huyo? Ni mke wa mtu
kweli?
Mke wa H-Baba, Flora Mvungi naye akamvaa Uwoya, akamchamba,
wakachambana. Mke wa mtu anagombana na mwanamke mwingine kisa mwanaume
tofauti na mumewe. Ninaposema hafai kwenye jamii namaanisha kweli.
Matukio
ambayo anakumbana nayo hususan hili la wizi wa simu, achukue kama
changamoto na ajisahihishe pale alipojikwaa. Amwangukie mumewe pengine
mambo yakamnyookea. Iwe kama ameiba yeye moja kwa moja au aliuziwa,
ajisahihishe.
Source:Global Publishers
No comments:
Post a Comment