Tukio hilo limetokea katika benki hiyo iliyoopo
katika makutano ya mtaa wa Indira Gandi na Mosque ambapo baadhi ya
mashuhuda wameelezea tukio hilo lilivyokuwa.
Akizungumza katika eneo la tukio kamanda wa polisi
mkoa wa Ilala kamanda Marieta Minagi amesema bado wanaendelea kufanya
uchunguzi wa tukio lenyewe ingawa mpaka sasa ni kama milioni zaidi 150
zinahisiwa kuibiwa.
Naye mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meki Sadiki
akiwa katika eneo hilo amesema matukio ya Kuiba fedha katika benki
yanazidi kushamiri na hivyo kuna haja ya taasisi husika kujipanga
upya.
Hata hivyo ITV ilishuhudia baadhi ya wafanyakazi wa
benki hiyo wakipandishwa katika gari la polisi lenye namba za usajili
T220 AMV na kuondoka nao kwa ajili ya mahojiano
No comments:
Post a Comment