Ukikutana na Ommy Dimpoz amevaa mkufu
mkubwa wenye muonekano wa weusi na almasi, tambua kuwa amevaa dola
10,000 sawa na shilingi milioni 17 shingoni.
Ommy akiwa amevaa mkufu aliozawadia na J-Martins (Picha: Gongamx)
Mkufu huo alizawadiwa jana na staa wa
Nigeria J-Martins kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa jana
iliyoendana sambamba na party ya East Meets West iliyofanyika Elements
Lounge.
J-Martins, Ommy Dimpoz na Man Walter
“Kiukweli mimi mwenyewe nilifarijika sana,” Ommy ameiambia Bongo5.
“Niliona jamaa hatukuishia kwenye
kufanya kazi lakini tumefanya kazi for the love, tumeongea vitu vingi
kuhusu mipango yetu ya video. Kikubwa zaidi nilifurahi sana, bado furaha
yangu ipo naona imekuwa ni kitu kikubwa kwangu, nafikiri wiki hii
imekuwa wiki nzuri sana,” ameongeza.
“Ni mkufu ambao una vitu vya kung’aang’aa, kwa msanii mkubwa kama yeye kunua mkufu wa dola elfu 10 anaweza kuafford.”
Kuhusiana na show yake ya kesho Jumapili
iliyopewa jina Tupogo Night, itakayofanyika Club Billicanas, Ommy
Dimpoz amesema watu wategemee surprise pia na show kali.
No comments:
Post a Comment