Kaka aambia Milan kutomlipa mshahara

Kaka
Mchezaji wa kiungo cha kati wa
AC Milan Kaka ameitaka kilabu yake kutomlipa mshahara wake huku
akiendelea kupona kutokana na jereha lake la paja ambalo alilipata
wakati wa mchezoo wake wa kwanza tangu kujiunga na kilabu hiyo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa timu ya Brazil
aliondolewa uwanjani na jeraha hilo katika dakika ya 70 ya mechi
waliyokwenda sare ya mabao mawili na timu ya Rossoneri.
Alirejea Milan bila malipo yoyote mapema mwezi huu baada ya kuhamia Madrid mwaka 2009 kwa kima cha pauni milioni 56.
"sitaki chochote kutoka kwa Milan , kwa sbaabu ya mapenzi yangu ya mchezo huu hadi nitakapopata afueni,'' alisema Kaka
''Na kwa sababu hii, nimeamua kutumia mshahara
wangu kwa kipindi hiki.Kile ambacho ningeomba tu ni kusaidiwa ili niweze
kupona vyema.''
"ni wakati mgumu kwangu lakini nimeanza kufanya kila niwezalo kupona, ninatumai nitapona haraka. ''
Kaka alisema kuwa alikuwa ameshauriana na makamu
wa rais wa kilabu hiyo Adriano Galliani na madaktari wa kilabu hiyo
kabla ya kukitaka kilabu kutomlipa.
Haijulikani ikiwa Milan imekubali ombi la mchezaji huyo.
Kaka, ambaye alishinda tuzo la mchezaji bora
zaidi duniani mwaka 2007 alichezea Milan katika mechi 268 na kuingiza
mabao 95 kati ya mwaka 2003 na 2009. Alisaidia kilabu hiyo kushinda ligi
ya Serie A mwaka 2004 na 2007 kwenye michuano ya mabingwa wa Ulaya.
Mnamo mwaka 2010, mlinzi wa Milan Oguchi Onyewu
alikubali kutia saini mkataba wa mwaka mmoja na kilabu hiyo bila malipo
baada ya kutochezeshwa kwa mwaka mmoja mfululizo.
No comments:
Post a Comment