Kaburi la mtu aliyekufa na baadaye kuonekana hai (msukule) lafukuliwa huko Geita.

 

Hatimaye kaburi la kijana Shabani Maulidi anayesadikika kufariki miaka mitatu iliyopita na wiki iliyopita kuonekana na mzazi wake akiwa hai limefukuliwa leo chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Maelfu ya wakazi wa Geita na viunga vyake walikusanyika nyumbani kwa mzazi wa shabani maulidi lilipo kaburi hilo kushuhudia ufukuaji wa viungo vya mtu anayedaiwa kufariki na kuzikwa, ambapo mtaalam wa maabara ofisi ya mkemia mkuu kanda ya ziwa Bwana Lucas Nduguru amesema kazi ya kuchunguza vipimo vya  vinasaba (DNA) vya kijana huyo pamoja na wazazi wake, itakamilika ndani ya wiki mbili hadi mwezi mmoja ili kuthibitisha ukweli wa kupatikana kwa mtu aliyekwishafariki akiwa hai.

Baadhi ya wananchi wamesema wameshangazwa na tukio hilo na kuiomba serikali kutoa majibu sahihi ili kujua ukweli wa jambo hilo.

kijana Shabani Maulidi anadaiwa kuwa alifariki mwaka 2011 na kuzikwa nyumbani kwao,  cha ajabu tarehe 28 mwezi wa nane mwaka huu mama yake mzazi alimkuta katika majaruba ya mpunga akiwa hai na mpaka sasa anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Geita.

Habari na mwandishi wetu  ROSE MWEKO

No comments: