Wananchi zaidi ya 200 Mvomero wavamia na kugawana heka 500 za mwekezaji.

 Zaidi ya wananchi 200 wa kijiji cha kibaoni wilayani mvomero mkoani morogoro hawana maeneo ya kulima baada ya serikali ya kijiji hicho kuuza maeneo ya mashamba zaidi ya ekari 500 kwa mwekezaji huku wananchi hao wakitishia kuandamana na kujichukulia sheria mkononi ya kuvamia na kugawana maeneo ya mashamba hayo

Wakizungumza wakati wakigawana mashamba hayo wananchi hao wamesema kuwa wamegawana mashamba kwa wananchi wote ambapo kila mwananchi amepata ekari mbili na kusema wanashangaa kuona mipaka inawekwa katika maeneo yao kuashiria kuuzwa kwa eneo hilo bila taarifa huku wakiendelea kukosa maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo hali inayopelekea kushindwa kulea familia zao.

No comments: